Wednesday Jun 19, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Kikwete azungumzia tatizo la ajira kwa vijana

1st June 2012
Print
Comments
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa afDB katika ukumbi wa AICC jijini Arusha jana.

Rais Jakaya Kikwete amesema wimbi kubwa la vijana wasio na ajira katika nchi za Afrika ni changamoto kwa nchi hizo na kama ufumbuzi usipopatikana haraka, serikali zilizochaguliwa kidemokrasia zinaweza kukubwa na machafuko kutoka makundi ya vijana.

Alisema hayo jana wakati akifungua Mkutano wa 47 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaoendelea jijini hapa.

Alisema tatizo la ukosefu wa ajira ni kubwa kwa nchi nyingi za Afrika na likiachiwa bila kutafutiwa ufumbuzi linaweza kuhatarisha usalama wa serikali zilizochaguliwa kidemokrasia.

“Hili ni jukumu la kila mmoja duniani kusaidia kumaliza tatizo hili…wapo watu wanadhani kwamba  tatizo lililotokea kwenye nchi za Kiarabu lilitokana na viongozi wa hizo kukaa muda mrefu madarakani, lakini ukweli ni kwamba tatizo hilo lilitokana na vijana wengi kukosa ajira,” alisema.

Alitaka nchi za Afrika kuwekeza katika ajira ya vijana kwa kushirikiana na taasisi za fedha kama vile AfDB na akaongeza, “Afrika inahitaji misaada ya kifedha na kiufundi.”

Alitaja maeneo kadhaa ambayo yanasababisha nchi za Afrika kurudi nyuma kuwa ni, ukosefu wa miundombinu bora, umeme wa uhakika na kilimo duni na akataka serikali kuwekeza katika masuala hayo.

Alitaka pia Afrika kuacha kuuza bidha ambazo hazijaongezewa thamani (malighali) kwani hazipati faida ya kutosha na huongeza ajira kwa nchi za nje.

Aidha, amezitaka nchi za Afrika kuzifikia nchi nyingine zilizoendelea katika elimu ya sayansi na teknolojia, hususan, teknohama.

“Lazima tuwafikie wenzetu katika sayansi na teknolojia, tunachotakiwa ni kuhakikisha tunawekeza katika elimu ya vijana wetu,” alisema.

Pia alizitaka alizitaka nchi za Afrika kuheshimu utawala wa sheria na utawala bora vikipewa kipaumbele nchi za Afrika zinaweza kuongoza duniani kwa kuwa na uchumi wenye nguvu.

Kuhusu ajira kwa vijana, Rais Kikwete, alisema hilo kwenye Mkutano huo ulihudhiriwa na Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, badala ya marais 10 waliotarajiwa.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment