Thursday May 5, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Jaji aonya walalamikaji dhidi ya Tundu Lissu

28th March 2012
Print
Comments
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema)

Jaji Moses Mzuna wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Singida, anayesikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), ameuonya upande wa walalamikaji kuhakikisha unawaandaa vyema mashahidi wao.

Alitoa angalizo hilo, kufuatia shahidi wa sita, Matheo Mnyambili, ambaye alikuwa wakala wa CCM kituo namba tatu katika Shule ya Msingi Makiungu, kuieleza Mahakama kuwa mgombea udiwani kupitia Chadema Kata ya Mungaa, Mateo Alex, alitoa rushwa ya chakula.

Shahidi huyo alidai kuwa Alex  aligawa chakula hicho kwa mawakala wanne, ikiwemo juisi, maji na biskuti, lakini hoja hiyo ilipingwa na Lissu, ambaye aliiambia Mahakama kuwa shahidi anakiuka taratibu, kwa sababu diwani huyo hayumo kwenye shitaka.

Awali Jaji Mzuna aliahirisha Mahakama kwa nusu saa, ili kutoa nafasi kwa walalamikaji  walioongozwa na wakili wao, Godfrey Wasonga, wakutane nje ya Mahakama na mashahidi wao na kwamba wafuate taratibu na sheria katika kuwasilisha ushahidi.

Baada ya muda huo kupita na Mahakama kuendelea, Mnyambili alianza kutoa ushahidi kwa kumtaja Alex, na kupingwa na Lissu, hali iliyomlazimisha Jaji Mzuna kutoa onyo hilo alilosema ni la mwisho kwa walalamikaji.

“Wasonga, muwe mnakutana na mashahidi wenu, mnakaa nao ili kuwaelekeza, sisi tunataka mashahidi wakija hapa waje kuthibitisha juu ya tuhuma,” alisema Jaji Mzuna na kuongeza:  “Hii iwe ni mwisho, tunataka waje waeleze kile walichoona siku hiyo.” Mnyambili alidai kuwa siku hiyo akiwa wakala wa CCM aliwaona mawakala wa NCCR-Mageuzi, TLP, Chadema na mmoja ambaye hakumbuki chama chake wakipewa chakula na alibaini hiyo ni rushwa, kwa sababu yeye hakupewa.

Alipoulizwa iwapo chama chake hakikumpatia chakula, shahidi huyo alidai kuwa baada ya siku tatu yeye na mawakala wa CCM walipatiwa Sh. 5,000 kila mmoja na chama chao. Lissu alimuuliza tena shahidi huyo iwapo alimuona yeye (Lissu) akigawa chakula hicho, ambapo Mnyambili alidai kuwa hakuwepo, ila baada ya diwani kutoka ndipo Lissu alifika kwenye kituo hicho.

Wasonga anawakilisha walalamikaji wawili, Shabani Itambu na Pascal Hallu, wanaopinga ushindi wa Tundu Lissu dhidi ya Jonathan Njau wa CCM.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles