Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Walimu wapuuza vitisho vya kukatwa mishahara

1st August 2012
Print
Comments
Raisi wa CWT Gratian Mukoba

Chama cha Walimu CWT (CWT) Mkoa wa Tanga kimesema tamko la serikali la kutaka walimu wote waliogoma wafutiwe mishahara halitakuwa kigezo kusitisha mgomo wao.
 
Akizungumza na NIPASHE, Katibu wa CWT Mkoa wa Tanga, Ndelamio Mangesho, alisema mgomo huo uliitishwa na CWT na siyo serikali hivyo walimu hawana sababu za kutishwa na kauli zinazotolewa.
 
“Mgomo huu utasitishwa pale tu ambapo Raisi wa CWT atawataka walimu kufanya hivyo na si vinginevyo,” alisema Mangesho.
 
Hata hivyo, aliwataka walimu kutambua kuwa mgomo huo ni halali na hawana sababu ya kuhofia vitisho vinavyotolewa na serikali.
 
Alisema wilaya zote za Mkoa wa Tanga zimekuwa na mwitikio mzuri katika mgomo huo kasoro Halmashauri ya Jiji la Tanga ambapo kuna baadhi ya walimu walifika shuleni.




 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment