Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Zimbabwe yaja leo kujipima na Twiga Stars

9th May 2012
Print
Comments
Kaimu Mkuu wa Wilaya wa Dodoma, Betty Mkwasa (kulia), akimkaribisha kwa kumkumbatia kocha wa timu ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars, Boniface Mkwasa "Master", ambaye ni mume wake, wakati timu hiyo ilipowasili jijini Dodoma jana kwa ajili ya mechi ya kirafiki.

Timu ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars, inatarajia kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya wenzao wa Zimbabwe kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi.

Awali Twiga Stars na Zimbabwe walitarajiwa kuumana Aprili 28 lakini wageni hao waliikacha Twiga na kuamua kucheza dhidi ya Zambia. Timu zote hizo zinajiandaa na mechi zao za kusaka tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake baadaye mwaka huu.

Akizungumza jana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa Zimbabwe inatarajia kuwasilia nchini leo jioni ikiwa na msafara wa watu 25.

Wambura alisema katika kujiandaa na mechi yake dhidi ya Ethiopia itakayofanyika jijini Addis Ababa Mei 26, Twiga Stars iko mkoani Dodoma na leo itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa huo ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 na baadaye itaelekea Mwanza kucheza mechi nyingine ya kirafiki itakayofanyika kesho.

Twiga Stars iliyo chini ya Kocha Mkuu, Boniface Mkwasa, ilianza vyema harakati za kusaka nafasi ya kushiriki fainali hizo za Afrika kwa mara ya pili baada ya kuifunga Namibia jumla ya magoli 7-2 wakati Ethiopia wao waliiondoa Misri.

Fainali hizo za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake mwaka huu zitafanyika nchini Equatorial Guinea.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles