Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Adaiwa kumbaka mtoto wa miaka sita

20th May 2012
Print
Comments

Mwanakijiji cha Emarti, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, amekamatwa akidaiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka sita.

Mtuhumiwa Maine Chomora (33) anadiwa kumvizia mtoto huyo barabarani na kumnajisi wakati alipotumwa dukani na wazazi wake nyakati za usiku .

Mwangalizi wa Haki za Binadamu wa Kijiji, Jackson Mwire, alisema alisikia kilio cha mtoto huyo akiomba msaada kwa watu ndipo wasamaria wema walipotoka nje na walipofika hapo wakamkuta mtuhumiwa akitenda kitendo hicho.

"Huwezi kuamini kwani vitendo hivi vimezoeleka hapa Emarti, kila tukiwakamata watuhumiwa baada ya muda mfupi huachiwa na polisi wakidaiwa kuwa hawana hatia, hali hii inatisha kijijini hapa," alisema Mwire. Alisema pamoja na kutolewa elimu kwa umma juu ya madhara ya ubakaji, jamii imekuwa ikikumbana na mkasa huu ambao wakati mwingine hofu imezidi kutanda kuwa huenda wanaofanya vitendo hivi wanasambaza Virusi vya Ukimw (VVU) .

Mwire alisema pamoja na mtuhumiwa kukutwa akitenda kosa hilo baada ya muda ataonekana akiwa huru mitaani huku akitamba jambo ambalo linawakatisha tamaa wananchi na wanaharakati.

Katika hatua nyingine, Mwire ameiomba Serikali pamoja na mahakama kusimamia sheria vizuri hasa pale wanapokamatwa watu juu ya matukio hayo na uchunguzi ufanyike haraka na kufikishwa mahakamani watuhumiwa ili haki itendeke.

Kwa upande wake, Maulidi Kijongo mwananchi wa wilayani Kiteto aliliambia gazeti hili kuwa moja ya sababu ya kutotokomezwa vitendo hivyo ni pamoja na kukithiri kwa rushwa kwa wasimamizi wa sheria hizo.

"Ukienda polisi na tatizo lako kuingia ni bure kutoka ni pesa hivyo ili hali hii iishe na kufanya vitendo hivi visiendelee lazima turudishe maadili ya Kitanzania ambayo awali yalikuwa msaada mkubwa kwetu," alisema Kijongo.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles