Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

`Bidhaa zisizo na ubora zipigwe marufuku nchini`

7th May 2012
Print
Comments

Serikali  imtakiwa kuzifuatilia kwa umakini na kuzipiga marufuku bidhaa zisizo na ubora zinazoingizwa nchini na wafanyabiashara waliokosa uzalendo kwa kuwa zinahatarisha maisha ya watu.

Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam  na Msajili wa Bodi ya Wahandisi  nchini (ERB), Injinia  Steven Mlote, kwenye hafla ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya kiyoyozi aina MULTI-V3, iliyohudhuriwa na washauri  pamoja na wadau wa ujenzi.

Injinia Mlote aliwaasa wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanaingiza bidhaa zenye ubora na zenye viwango nchini, ili kuliepusha taifa kuwa dampo la bidhaa feki.

“Wafanyabiashara waliokosa uzalendo, wanaingiza bidhaa feki ambazo zinahatarisha maisha ya Watanzania, inatakiwa serikali kuzifuatilia bidhaa hizo kwa umakini na kuzipiga marufuku” alisema Mlote.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles