Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Vigogo watimuliwa Tazara

26th April 2012
Print
Comments

Bodi ya Shirika la Reli Tanzania na Zambia (Tazara), imewafukuza kazi vigogo saba kwa sababu ya kuvurunda na kuwaweka viporo Mkurugenzi Mkuu na Kaimu wake hadi Baraza la Mawaziri wa nchi hizo litakapokaa kujadili na kutoa uamuzi ya hatma yao.

Akizungumza na wafanyakazi wa Tazara jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, alisema kutokana na sheria ya Tazara ya mwaka 1965 inaainisha majukumu kwa Baraza la Mawaziri na kuwa kazi yake ni kutoa mwongozo kwa mambo yanayohusu Bodi ili itekeleze, lakini pia kulingana na sheria ya mwaka 1995 kifungu cha 12(2), bodi inapewa mamalaka ya kutengua au kumteua Mkurugezi kwa kuwa yeye (Mkurugezi) jukumu lake ni kusimamia utendaji.

“Lazima hatua zichukuliwe kwa wale wote ambao taarifa za moja kwa moja kutoka kwenye ripoti ya mahesabu zinazoonyesha kuwa kiasi cha Dola milioni 12 zimepotea na hawa viongozi wamehusika na hasara hiyo, huu ni ubadhirifu ambao hauwezi kuvumiliwa, lakini kwa kupande wa Mkurungenzi na Kaimu wake nasubiri waziri mwenzangu wa Zambia tukae na kujadili,” alisema.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles