Monday May 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Yanga yaacha nyota 11

29th June 2012
Print
Comments
  Wamo Asamoah, Mwape, Kado
Afisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu

Mabingwa  watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Yanga wametangaza kuwaacha wachezaji 11 katika usajili wa msimu ujao; wakiwemo Mghana Kenneth Asamoah, Mzambia Davis Mwape na kipa Shaaban Kado waliyempeleka kwa mkopo katika timu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Afisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu, aliwataja wachezaji wengine walioachwa na timu hiyo kuwa ni Julius Mrope, Idd Mbaga, Atifu Amour, Godfrey Bonny, Mohamed Mbegu, Abuu Ubwa na Zubery Ubwa.

Aliongeza kuwa Mwape na wenzake wameachwa kutokana na sababu mbalimbali, baadhi zikiwa ni kumalizika kwa mikataba na wengine ni kushuka kwa viwango vyao.

Alisema mbali na Kado, wapo wachezaji wengine kadhaa ambao pia watauzwa kwa mkopo ili wakapate nafasi ya kuzichezea timu nyingine mbalimbali za ligi kuu na kwamba, majina yao yanatarajiwa kujulikana leo baada ya uongozi wa klabu hiyo kuyawasilisha kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

"Tutawasilisha TFF majina yote ya wachezaji tuliowaacha na kuwauza kwa mkopo," alisema Sendeu.

Katika hatua nyingine, Sendeu alisema kuwa wachezaji wengine wa timu yao wanaendelea vyema na mazoezi kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame, wakiwa chini ya kocha Fredy Felix Minziro; isipokuwa kiungo Nurdin Bakari na kipa Yaw Berko ambao ni majeruhi.

KUIVAA EXPRESS


Wakati huohuo, Yanga watashuka dimbani kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kucheza dhidi ya  Express ya Uganda.

Sendeu alisema kuwa wageni wao Express walitarajiwa kuingia jijini Dar es Salaam jana usiku, wakiwa na msafara wa watu 26.

Sendeu alisema katika kuhakikisha kuwa maandalizi yao yanakwenda vizuri kabla ya michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14, makatibu na wenyeviti wa matawi ya Yanga watakutana leo jioni kwenye makao makuu ya klabu hiyo kujadili mwenendo wa timu yao.





 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment