Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Tanesco yasema hali ni mbaya

10th May 2012
Print
Comments
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), linahitaji  Sh. tilioni 1.3 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya usambazaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Kadhalika, Tanesco limetangaza kuwa hali ya maji katika mabwawa yake ya kuzalisha umeme ni mbaya na kwamba kama litategemea chanzo hicho pekee uzalisjhaji utasitisha ifikapo Agost mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, William Mhando, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari. Alisema ikiwa serikali itawasaidia kiasi hicho cha fedha wataweza kuimarisha miundombinu ya usambazaji wa umeme na hivyo kusaidia kupata umeme wa uhakika.

Alisema miundombinu ya nguzo na mitambomingine imechoka na kwamba hatua hiyo imetokana na serikali kuliacha shirika hilo kwa muda mrefu bila kuweka fedha wakati ilipokuwa ikisubiri kulibinafsisha.

Aidha, Mhando alisema mchakato wa kupata mkopo wa Sh. bilioni 408 umefikia hatua za mmwisho na kwamba muda wowote fedha hizo zitatolewa.

Kuhusu hali ya maji katika mabwawa mbalimbali hapa nchini, Mhando alisema kina chake kimepungua.
Bwawa la  Mtera alisema kina  cha juu cha  maji kinachotakiwa ili kuzalisha umeme ni ujazo wa mita 698.5 kutoka usawa wa bahari na cha chini ni mita za ujazo 690 kutoka usawa wa bahari.

Alisema kwa sasa bwawa hilo lina ujazo wa mita 691.36 kutoka usawa wa bahari na kwamba kimeabaki kiasi kidogo kufikiwa ili kusitisha uzalishaji wa umeme katika chanzo hicho. “Bwawa likifikia mita za ujazo 690 kutoka usawa wa bahari inatakiwa uzalishaji wa umeme usitishwe ama tupate kibali maalum cha serikali,” alisema.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles