Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Kagame Cup yapigwa kalenda

1st June 2012
Print
Comments
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye

Mashindano ya kuwania ubingwa wa nchi za Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame ambayo yalitarajiwa kufanyika kuanzia Juni 23 hadi Julai 8 hapa nchini sasa yamesogezwa mbele hadi itakapotangazwa tena, imefahamika.

Wenyeji Tanzania Bara watawakilishwa na timu tatu ambazo ni pamoja na mabingwa watetezi Yanga, Simba na Azam ambayo msimu uliopita imemaliza ikiwa katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu ya Bara.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye, alisema kuwa mabadiliko yaliyofanyika yanatokana na majukumu yanayozikabili timu za taifa.

Musonye alisema kuwa sekretarieti ya CECAFA bado inakutana kupanga wakati muafaka utakaofaa ili mashindano hayo yaweze kufanyika kwa sababu ni muhimu kwa malengo ya kuwapa nafasi wachezaji kuonyesha vipaji vyao kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi za nchi wanazochezea.

"Mashindano yatakuwepo, ila yataanza lini bado haijajulikana, wiki ijayo ndio tutakuwa kwenye wakati mzuri wa kutangaza kila kitu," alisema Musonye.

Musonye alisema kuwa CECAFA inataka kuona wanachama wake wote wanafanya vizuri katika mbalimbali ya kuwania tiketi za kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani na Kombe la Dunia mwaka 2014.

Idadi kubwa ya wachezaji wa klabu zinazotarajiwa kushiriki katika Kombe la Kagame wako katika timu za taifa za nchi 12 za ukanda huu ambazo zitacheza mechi zake za kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia Juni 17 ikiwa ni siku chache kabla ya tarehe iliyokuwa imetangazwa awali ya kuanza kwa michuano hiyo.

Musonye alisema michuano hiyo itakuwepo pamoja na Kombe la Chalenji ambayo bingwa mtetezi ni Uganda.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment