Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mafuriko yaacha watu 100 bila makazi

30th April 2012
Print
Comments

Zaidi ya nyumba 210 zimeharibiwa kwa kusombwa na kubomolewa na mafuriko na watu zaidi ya 100 kukosa mahali pa kuishi kufuatia mvua kubwa kunyesha wilaya ya Maswa mkoani Simiyu na kusababisha mafuriko katika baadhi ya vijiji vya kata ya Malampaka na Buchambi Tarafa ya Sengerema.

Aidha, takribani hekta 170 za mazao ya mpunga na pamba zimeharibiwa na tani 40 za vyakula mbalimbli zikiwemo nafaka kuharibiwa huku kuku na bata wakisombwa na mafuriko hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, James Yamungu, aliiambi NIPASHE jana kuwa mafuriko hayo yamesababishwa na mito iliyoko katika maeneo ya kata za Malampaka na Buchambi katika vijiji la Lali,Kizungu na Zawa kujaa maji.

Alisema zaidi ya watu 100 hivi sasa hawana mahali pa kuishi huku hekta 90 za mpunga na hekta 78.5 za pamba na chakula zikiwa zimeharibiwa kabisa na kuhitaji msaada wa haraka wa kibinadamu kwa wananchi hao.

Yamungu alisema kuwa mapema wiki iliyopita mvua kubwa ikiambatana na upepo mkali ilinyesha wilayani Maswa katika tarafa ya Sengerema  na kusababisha mto mkubwa wa Mwashinida na Malampaka na mto mdogo wa Malampaka kufurika maji na kusababsiha maaafa hayo.

Alisema bado serikali haijaanza kutoa msaada wowote licha ya ofisi yake imeanza tathimini na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa
Simiyu na kitengo cha Mafaa ofisi ya Waziri ,kuu zimearifiwa juu ya maafa hayo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles