Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Red Cross kuelimisha matumizi sahihi ya nembo

4th May 2012
Print
Comments
Adam Kimbisa

Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania kitazindua kampeni ya matumizi sahihi ya nembo yake wiki ijayo.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Adam Kimbisa, alisema jana kuwa lengo la kampeni hiyo itakayozinduliwa Jumanne  ni kulinda matumizi sahihi ya nembo ya Red Cross ambayo imekuwa ikitumiwa na watu wasiohusika.

“Tatizo inatumika vibaya kwa mfano utakuta mtu mwenye kiduka cha kuuza dawa anaweka nembo ya Red Cross. Inatakiwa itumike kama kinga wakati wa vita na migogoro ili kuwakinga waathirika wa vita, kulinda watumishi wanaojitolea wakati wa vita,” alisema Kimbisa.

Kimbisa alisema kisheria mashirika yanayoruhusiwa kutumia nembo hiyo ni Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC), Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali nnyekundu (IFRC) na wahudumu wa afya wa kijeshi na vifaa vyao.

Ofisa wa red Cross Tanzania, Julius Kejo, alisema kuwa sheria iliyoanzisha chama hicho nchini baada ya uhuru inailinda nembo hiyo dhidi ya matumizi yasiyo sahihi na kuongeza kuwa hata hivyo, sheria hiyo imepitwa na wakati kwa kuwa kiwango cha adhabu inayotolewa kwa matumizi yasiyo sahihi ni kifungo kisichozidi miezi sita au faini isiyozidi Sh. 1,000 na kwamba wako katika mchakato wa kutaka sheria hiyo ifanyiwe marekebisho.

Naibu Mkurugenzi wa chama hicho,Peter Mlebusi, alisema katika kampeni hiyo wataelimisha umma kuhusu matumuzi sahihi ya nembo hiyo kupitia vyombo vya habari na mchakato walioanzisha wa kubadili sheria.

Ofisa wa Mawasiliano wa chama hicho, Raymond Kanyambo, lisema nembo hiyo imekuwa ikitumiwa katika zahanati, maduka ya dawa, magari ya kubeba wagonjwa, katika daladala na bajaj.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles