Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

SSRA yasifu ripoti ya CAG, Kamati ya Bunge

2nd May 2012
Print
Comments
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh

Mamalaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imempongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, na kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC) kwa ripoti zake nzuri kuhusu matumizi mabaya katika mifuko ya hifadhi ya jamii nchini, na kwamba iko katika mchakato wa kushughulikia hali hiyo.

Akizungumza na NIPASHE  iliyotaka kujua SSRA inafanya nini kutokana na ripoti ya CAG ya kuwako kwa fedha nyingi za mifuko hiyo ambayo imekopwa na kuwekezwa na serikali sehemu mbalimbali, lakini ulipaji wake umekuwa si wa kutia moyo kitu inachoweza kuathiri fedha za wanachama, Meneja wa Mawasiliano wa SSRA, Sarah Kibonde, alisema SSRA kwa sasa inajikita katika kuweka miongozo katika uwekezaji na usimamizi ili kuhakilisha fedha za wanachama zinakuwa salama.

“Sasa hivi tunaajiri mameneja wa fedha na wasimamizi (fund managers and custodian) kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya SSRA,” alisema Kibonde na kuongeza kuwa mwongozo wa utekelezaji kazi hizo umekwisha kumalika na kutiwa saini na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na utazinduliwa rasmi hivi karibuni.

Alisema kazi za miongozo hiyo itazingatia zaidi usimamizi wa vitegauchumi, kumbukumbu za wanachama, ili kuhakikisha kuwa uhai wa mifuko hiyo unabakia salama wakati wote.

Hata hivyo, Kibonde alisema uhai wa mifuko hautegemei tu uwekezaji, lakini pia akiba na wingi wa wananchama.

Kwa mujibu wa sheria ya SSRA ya mwaka 2008 majukumu yake ni pamoja na kusajili mameneja na wasimamizi wa mifumo.

Aidha, kazi nyingine ya Mamlaka hiyo ni kudhibiti na kusimamia utendaji wa mameneja na wasimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kazi nyingine ya SSRA ni kuweka utaratibu wa uendeshaji katika sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii, kulinda na kusimamia usalama wa maslahi ya wanachama.

Kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuhamasisha na kuendeleza sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii, kumshauri Waziri kuhusu sera na mambo ya uendeshaji kuhusu sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii

Kazi nyingine ya SSRA ni pamoja na kuweka sheria pamoja na kuangalia utendaji wa kila siku wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

Nyingine ni kutoa elimu, kupendekeza, kuratibu na kuleta mabadiliko katika sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii; kuteua msimamizi wa mfumo kama ni lazima, kuwezesha upanuzi wa mifuko ili kuyafikia makundi yasiyokuwa rasmi na uanzisha programu ya kuelimisha umma na kuhamasisha kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii.

Katika ripoti ya CAG ya mwaka 2010/11 ilibainisha maeneo yenye matatizo katika mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa ni pamoja nafedha za wanachama kuwa hatarini.
Mifuko iliyotajwa kuwa hatarini kufilisika ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma (PPF), Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) NA Mfuko wa  Bima ya Afya (NHIF).

Ripoti ya CAG ilibani kuwa NSSF ilitoa Sh. bilioni 234.1 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), lakini mkataba uliosainiwa ni wa Sh. bilioni 35.2.

Mbali na mradi wa Udom, pia serikali haijalipa deni la ujenzi wa ukumbi wa Bunge ambapo NSSF inaidai Sh. bilioni 19.77, PPF Sh. bilioni 7.9 na LAPF Sh. bilioni 2.91.

Kadhalika, NSSF ilitoa Sh. bilioni 5.33 na riba ya asilimia 15 kwa miaka 10 zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa taasisi ya serikali ya kiusalama mwaka 2007, PPF katika taasisi hiyo iliwekeza Sh. bilioni 6.4.

Fedha nyingine Sh. bilioni 20 za NSSF zilikopeshwa kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba a polisi na Sh. bilioni 12.9 zilikopeshwa kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mwaka 2007 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Machinga Complex.

Kwa upande wa jengo la Machinga Complex hadi kufikia Juni 30, 2011 mkopo na riba ulikuwa umefikia Sh. bilioni 15.3

Ripoti ya CAG ilibaini kuwa mikopo mingine hailipwi kulingana na mikataba ya mifuko hiyo bila kutaja viwango kuwa ni ile iliyotolewa kwa kampuni ya Continental Venture (T) Limited, Meditech Industrial Co Ltd , General Tyre, Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu HESLB na mgodi wamakaa ya mawe wa Kiwira.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles