Saturday May 18, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Ngeleja afunguka

4th June 2012
Print
Comments
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amevunja ukimya na kusema hajawahi kwenda jimboni na kupokelewa kwa mbwembwe na wapigakura wake, kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Ngeleja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema (CCM), alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa na NIPASHE jana kuzungumzia taarifa hizo.

Alisema anashangazwa na kuhuzunishwa na taarifa hizo kwa kuwa hazina ukweli wowote na zimekuwa zikiwapotosha wananchi.

“Tangu Baraza la Mawaziri livunjwe sijawahi kwenda jimboni na kupokelewa kwa mbwembwe kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii,” alisema Ngeleja.

Alisema baada ya kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri mwezi uliopita, amekuwa akiendelea na vikao vya Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo, ambayo ameteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wake.

Ngeleja alivitaka vyombo hivyo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuacha kutangaza taarifa za uzushi kwamba amekwenda jimboni na kupokelewa kwa mbwembwe, kwani hazina manufaa yoyote, badala yake zinaupotosha umma.

Hata hivyo, alisema muda wa kwenda jimboni bado haujafika na kwamba, ukifika atakwenda kama ilivyo desturi kwa wabunge kuzungumza na wapigakura wao juu ya mambo yanayohusu maendeleo ya jimbo na taifa kwa jumla.



 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment