Sunday May 19, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Wazee wachukua timu Yanga

29th April 2012
Print
Comments
  Kutangaza kamati ya muda kesho
Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga

Mwenyekiti wa Yanga ambaye alikuwa katika shinikizo kubwa la kujiuzulu nafasi hiyo kufuatia matokeo mabaya kwenye ligi kuu ya soka ya Bara kwa miaka 24 Lloyd Nchunga, amekabidhi timu kwa Baraza la Wazee kunzia jana.

Alipoulizwa Nchunga juu ya taarifa hiyo ya timu kuchukuliwa na wazee wa klabu, alikiri jana.

Akizungumza na Waandishi wa habari klabuni Yanga jana, katibu wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo Ibrahim Akilimali alisema:

Kufuatia kikao cha pamoja cha wazee wa klabu hiyo na Nchunga kilichofanyika Alhamisi, mwenyekiti huyo amekubali kuikabidhi timu kwa wazee ambao wataisimamia mpaka hapo hali ya mambo ndani ya klabu hiyo yatakapotulia.

Wazee hao kesho wanategemea kutangaza kamati maalumu ya muda itakayoiendesha timu hiyo.

Hatua hiyo, hata hivyo, ni kinyume na katiba ya Yanga na ya shirikisho la soka, TFF, hivyo kufanya makabidhiano hayo kuwa batili.

"Baada ya kupambanua mambo na kuona jinsi timu yetu inavyokwenda, kwenye kikao chetu na mwenyekiti tumekubaliana na kutoka na azimio moja la timu kuwa chini ya Wazee kwa kipindi chote mpaka hapo mambo yatakapokaa sawa," alisema Akilimali.

Yanga ambayo haijawahi kumaliza nje ya timu mbili za kwanza Bara tangu 1988 ikiwa bado inaitwa ligi daraja kwanza, ni mshindi namba tatu mteule kutokana na kupungukiwa angalau pointi nne kuwa katika nafasi ya kuikamata Azam iliyo katika nafasi ya pili.

Akilimali alibainisha mambo matatu ambayo yamechangia kuichukua timu kuwa ni kitendo cha kupokonywa ubingwa bila sababu ya msingi huku akielezea kuwa utovu wa nidhamu ndio sababu pekee iliyopelekea timu yao kupoteza ubingwa.

Sababu ya pili iliyotajwa na Baraza hilo la wazee ni kuchoshwa na hali ya klabu hiyo ya kutokuwa na uwezo wa kusafiri kutoka kituo kimoja kwenda kingine kwenye michezo ya ligi kuu.

Akilimali alisema Yanga imepata aibu kubwa ilipokwenda Arusha wiki iliyopita kucheza na JKT Oljoro ambapo baada ya mchezo walishindwa kulipa gharama za hoteli waliyofikia.

Deni hilo lilisababisha meneja wa timu Hafidh Salehe kushikiliwa na wamiliki wa hoteli huku wachezaji wakitoroka kurudi Dar es Salaam kwa gharama zao, alisema.

Alisema wanamshukuru Nchunga kwa mambo yote aliyoifanyia klabu hiyo na kumpongeza kwa hatua yake ya kuikabidhi timu kwa wazee hao.

Aidha, alisema kuwa wazee hao watayarithi madeni yote ya klabu hiyo yalikuwa chini ya Nchunga na ambayo yanatambulika kisheria.

"Ndugu zangu sisi hatujakurupuka, tumejipanga na tutaanza kulipa madeni yote ya klabu ambayo yanatambulika likiwemo deni la kocha wetu (Kostadin) Papic ambaye anatudai," alisema Akilimali.

Papic anaidai Yanga sh. milioni 24.7 za mshahara wa miezi mitatu.

Hata hivyo, habari ambazo si rasmi zinadai kuwa wazee wa klabu hiyo walimshinikiza Nchunga kupima mwenyewe kujiuzulu au kuikabidhi timu hiyo kwa wazee ili kuinusuru kuendelea kudorora.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment