Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

CCM yatangaza vita kwa watakaotoa rushwa

16th May 2012
Print
Comments
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye

Halmashauri Kuu (Nec) ya Chama cha Mapinduzi (CCM),  imebaini tishio la rushwa katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

Hayo yalisemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, wakati akizungumza na waandishi wa habari jana.

Nape alikuwa akielezea maamuzi yaliyofikiwa katika kikao cha Nec kilichomalizika juzi usiku na kusema mgombea atakayethibikika kuwa ameshinda uchaguzi kwa njia ya rushwa, atanyang’anywa ushindi alioupata.

“Pia atazuiwa asigombee tena katika uchaguzi mwingine wowote kwa muda utakaoamuliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa au atapewa adhabu kubwa zaidi ya hiyo kama itakavyoonekana inafaa,” alisema.

Alisema Nec imetoa maagizo kuwa kuanzia sasa ni marufuku kwa mgombea wa ngazi yoyote kuzunguka  matawini, kwenye kata, wilayani  na mikoani kukutana na wajumbe wa mkutano wa kumchagua kwa visingizio vya kuwasalimu wajumbe, kuwapa nauli au kujitambulisha.

“Mgombea atakayethibitika anazunguka ama amazunguka ataondolewa bila kuchelewa katika orodha ya wagombea,” alisema. Aidha, alisema watendaji na viongozi wa chama wa ngazi zote kuanzia sasa ni marufuku kuwatembeza wagombea ndani ya maeneo yao kwa nia ya kuwatambulisha kwa wapiga kura.

“Mtendaji au kiongozi atakayebainika anakiuka agizo hili atachukuliwa hatua za kinidhamu,” alisema na kuongeza kuwa kuanzia sasa ni marufuku kwa watendaji wa ngazi zote kuwaitia wagombea wajumbe wa mikutano ya uchaguzi kwa lengo lolote lile, kwani vikao vya aina hiyo ni haramu vinavyopalilia rushwa.

Nape alisema Nec iliazimia serikali iwahimize waajiri wahimizwe kupandisha mishahara na malipo mengineyo kwa wafanyakazi wao ili waweze kumudu gharama za maisha.

‘Serikali iweke jitihada zaidi katika kudhibiti ulanguzi wa bidhaa muhimu na upandishaji holela wa bei za vyakula, kodi na nyumba za usafiri.

Alisema kuwa kumekuwa na upandishaji holela wa bei za nyumba huku wamiliki wakitaka wapangaji kulima kodi ya miezi sia. Alisema jambo hilo linawafanya wananchi kutafuta fedha kwa njia nyingine kwa kuwa vipato vyao ni vidogo kuweza kumudu gharama.

Alisema Pia Nec imeagiza serikali kuchukua hatua za haraka za muda mfupi ikiwemo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT katika sukari. Aidha , Nec imeshauri utaratibu wa ruzuku ya mbegu na mbolea upanuliwe ili kunufaisha wakulima wengi.

Nape alisema serikali imeagizwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mpango wake wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula nchini hasa kwa kupitia Hifadhi ya Nafaka ya Taifa, (SGR), ikiwa ni pamoja na kujenga maghala zaidi ya mazao ya chakula katika maeneo ya uzalishaji wa mazao.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles