Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

NIDA yawaonya wanaouza fomu za usajili

23rd May 2012
Print
Comments
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Dickson E. Maimu

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imesema kuwa fomu za usajili wa vitambuilisho vya taifa haziuzwi na imeonya wanaofanya mchezo huo.

Taarifa ya NIDA iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana ikimnukuu Mkurugenzi Mkuu wake, Dickson E. Maimu, alisema kuwa wamepokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa katiba baadhi ya mikoa kuna watu wanauza fomu hizo, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Kumekuwepo taarifa kwenye baadhi ya mikoa nchini, kwamba fomu za usajili na utambuzi wa watu zenye lengo la kuchukua taarifa za wananchi na hatimaye kuwapatia Kitambulisho cha Taifa, kuanza kuuzwa  kinyume na taratibu, “ ilisema taarifa hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema vitendo hivyo vinalenga kuwahadaa wananchi na hivyo kuwataka wawe waangalifu na kuwafichua wale wote wanaojihusha na uuzaji huu, ambao ni kinyume cha taratibu, kanuni na Sheria ya Usajili.

“Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA), haijaanza kutoa fomu zozote za usajili kwa wananchi wa mikoani, zaidi ya mazoezi ya usajili kwa watumishi wa Umma kwa Dar-as-salaam, na Zanzibar, na zoezi la majaribio wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro lililofanyika mwezi Machi mwaka huu. Usajili rasmi wa wananchi kwa jumla unakusudiwa kuanza mapema mwezi Juni mwaka huu, kwa kuanzia na mkoa wa Dar-es-salaam,” ilifafanua taarifa hiyo.

Mwaimu alisisitiza kuwa kwa mujibu wa taratibu zilizoko NIDA inatoa fomu za za Utambuzi na Usajili wa Watu bure, kadhalika kitambulisho pia kitatolewa bure kwa wananchi.

Alisema utaratibu wa ugawaji fomu utatangazwa kwa wananchi wakati utakapowadia kupitia vyombo vya habari na aliwataka wananchi kutoa taarifa ya vitendo vya ukiukaji wa tarabu hizo kwenye kituo chochote cha polisi kilichoko karibu. Wananchi wa mikoani wametakiwa kuvuta subira kwani mchakato wa vitambulisho ukianza watajulishwa.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles