Wednesday Jun 19, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Wake wa maafisa JWTZ watoa msaada Lugalo

29th July 2012
Print
Comments

Maafisa na wake wa maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Shilingi milioni mbili kwa wanawake na watoto waliolazwa hospitali ya jeshi Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti Msaidizi wa Umoja wa wake wa maafisa toka Makao Makuu ya Jeshi hilo (UWAMA), Aikael Mrema, alisema jana kuwa, msaada huo ni sehemu ya majukumu ya umoja huo ulioanzishwa miaka miwili iliyopita.

Aikael alisema kuwa wameamua kusaidia kundi hilo la wanawake na watoto kwa sababu wamekuwa wakitegemewa na familia katika malezi.

Alitaja baadhi ya vitu walivyotoa kwa wagonjwa kuwa ni pamoja na sabuni, miswaki na dawa za meno, neti, machungwa pamoja na mizani ya kupimia uzito kwa kina mama wajawazito na watoto.

Naye, Katibu Msaidizi wa umoja huo, Lucy Issaru, alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo hospitalini hapo ili kumuunga mkono mkuu wa majeshi ambaye ndiye aliyehamasisha kuanzishwa kwa kikundi hicho.

Alisema mikakati waliyonayo ni kuwafikia watu wenye uhitaji kwenye jamii ili kuweza kuwasaidia kwa kuwapa misaada tofauti.

Akizungumza kwa niaba ya wajawazito waliolazwa hospitalini hapo Magreth Mtabuzi, aliupongeza umoja huo kwa kutambua umuhimu na mahitaji ya wagonjwa na kuamua kuwapatia msaada huo.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment