Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mahakama yatupa kesi ya Leticia Nyerere

24th May 2012
Print
Comments
Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere (CHADEMA)

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimepokea nakala ya hukumu ya kesi mbili zilizofunguliwa Marekani dhidi ya Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere, zenye kuonyesha mahakama imetupilia mbali kesi hizo.  

Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya Chadema ilieleza kuwa kwa mujibu wa Leticia, waliofungua kesi hiyo waliingia mitini baada ya kubainika kwamba kesi hiyo ilikuwa ni ya kutengenezwa kwa malengo ya kumchafua hali ambayo ingeweza kuwatia hatiani wahusika kwa kuwasilisha madai ya uongo.  

Taarifa hiyo ilieleza kuwa pamoja na kutupiliwa mbali kwa kesi hizo, mamlaka husika za Marekani zinaendelea na uchunguzi wa kumsaka aliyetoa madai kwamba Leticia amekamatwa na kutaka wananchi wamchangie fedha kwenye akaunti iliyotajwa katika ujumbe uliosambazwa kwa njia ya mtandao.  

“Hukumu hii inadhihirisha tahadhari niliyoitoa kwa wanahabari Mei17, 2012 ya kuwataka kusubiri maelezo rasmi kutoka kwa Leticia Nyerere na yatokanayo mahakamani kutokana na tuhuma zilizosambazwa kwenye mitandao kuwa na mwelekeo wa siasa chafu kukwaza jitahada zake na viongozi wa Chadema kutokana na kazi walizozifanya za kuwezesha watanzania waishio Marekani kuunga mkono mabadiliko,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika.  

“Chama kinaendelea kufuatilia kwa karibu suala hili na taarifa zaidi zitatolewa kwa umma katika hatua za baadaye kadiri iwezekanavyo.”

Kwa mujibu wa nakala ya hukumu ya kesi hiyo iliyotolewa Mei 22 na jaji R. Russelle Sadler Mahakama ya Wilaya huko Maryland. 

Wakati huo huo, Chadema kiwakumbusha Watanzania wanaoishi Marekani kuhudhuria kwa wingi katika Mkutano wa chama hicho utakaofanyika Maryland Mei 27, mwaka huu na kuwasiliana na Leticia kupitia [email protected] kwa maelezo zaidi.  
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles