Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

SBL,NMB wamwaga mamilioni Twiga Stars

24th May 2012
Print
Comments
Timu ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars

Timu ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars, ambayo inajiandaa na mechi za kufuzu kwa fainali zijazo za Afrika, jana ilipokea msaada wa Sh. milioni 30 pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo kutoka kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na benki ya NMB.

Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru, alisema kuwa sababu ya wao kutoa mchango huo ni kutambua umuhimu wa timu hiyo ambayo inalitangaza vyema jina la Tanzania nje ya nchi na pia jukumu la kusaidia maendeleo ya michezo ambalo ni kwa taasisi na makampuni mbalimbali.

Mafuru alisema kuwa Twiga Stars wameonyesha njia na wana mwelekeo hivyo milango kwa makampuni mengine iko wazi kuwasaidia ili waweze kutimiza ndoto zao.

Naye Mkurugenzi wa Masoko wa NMB, Imani Kajula, alisema kuwa wametoa mchango huo ili kuleta hamasa zaidi kwa wachezaji wa timu hiyo wafanye vizuri na wamefungua akaunti maalumu ya kuichangia timu hiyo ili iweze kufuzu kwa mara ya pili.

Naibu mkurugenzi wa michezo nchini, Juliana Yassoda, aliwashukuru SBL na NMB kwa msaada waliotoa na kuongeza kuwa wameonyesha mfano wa kuigwa.

Kocha Msaidizi wa Twiga Stars, Nasra Juma Mohammed, aliahidi timu hiyo itafanya vizuri na wanaishukuru pia serikali kwa kutoa posho kwa wachezaji na viongozi wote wa benchi la ufundi.

Twiga Stars itacheza mechi yake hiyo ya kwanza wenzao wa Ethiopia Jumapili ya Mei 27 na watarudiana Juni 16 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Itaondoka leo jioni kwenda Addis Ababa.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles