Wednesday Jun 19, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Minziro aipa Yanga Kombe la Kagame

24th June 2012
Print
Comments
Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro

Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro, amesema ana imani kubwa na timu hiyo itatetea ubingwa wa Kombe la Kagame la klabu bingwa ya Afrika Mashariki na kati mwezi ujao kutokana na usajili mzuri ambao umefanyika.

Aidha, akizungumza na Nipashe jumapili jana, Minziro alisema Yanga itatea ubingwa huo kutokana hali ya hewa klabuni hapo kutulia.

Alisema ujio wa wachezaji wapya na hali ya mambo klabuni hapo kutulia kunawapa matumaini ya kufanya vizuri.

"Ukweli timu haikufanya vizuri msimu uliopita kwa sababu ya malumbano miongoni mwa viongozi na mgogoro wa wanachama vilivyopelekea wachezaji kutokuwa na ari ya kushindana," alisema na kueleza zaidi:

"Lakini sasa mambo yametulia na unaweza kuona hata kwenye usajili wetu... nina uhakika timu itafanya vizuri kwenye Kagame na kwenye ligi."

Katika hatua nyingine, Minziro alisema yupo tayari kufanya kazi na kocha yoyote atakayeletwa na uongozi wa klabu hiyo.

Uongozi wa Yanga upo kwenye mchakato wa kusaka kocha wa kuziba nafasi ya Kostadian Papic aliyemaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu uliopita.

Mmoja wa wanachama wa Yanga anayejihusisha na usajili wa klabu hiyo, Seif Ahmed, alisema wanategemea kumpokea kocha mpya kesho Jumatatu.

Bila kufafanua jina Seif alisema wapo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na kocha huyo.

Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya Yanga zilisema klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na mwalimu wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Jacob Mulee.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment