Tuesday May 3, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Dk. Mwanjelwa: Sitii kutoteuliwa kuwa waziri

8th May 2012
Print
Comments
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, amesema hajutii kutoteuliwa kuwa waziri kwani alichaguliwa na wananchi wa mkoa huu ili aweze kuwatumikia kwa kuwaletea maendeleo akiwa katika nafasi yake ya ubunge na siyo mpaka awe waziri.

Amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kufuatia baadhi ya vyombo vya habari (siyo Nipashe) kumnukuu kuwa amejisikia vibaya kutoteuliwa kuwa waziri katika baraza jipya la mawaziri lililotangazwa Ijumaa iliyopita na Rais Jakaya Kikwete .

“Siwezi kulalamika kwa kutoteuliwa kuwa waziri, wananchi wa mkoa wa Mbeya walinichagua kuwa mbunge ili niwatumikie kwa nafasi yangu ya ubunge, isitoshe uamuzi wa kumteua mbunge kuwa waziri ni wa Rais mwenyewe, ifahamike kuwa sikwenda bungeni ili nichaguliwe kuwa waziri,” alisema.

Dk. Mwanjelwa alisema watu wanaomzushia kuwa anataka kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ni mahasimu wake wa kisiasa ambao wanataka kumchafua na kwamba kamwe hawezi kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kwenda upinzani.

Alisema hawezi kuihama CCM kwa sababu anatambua kuwa ndicho chama pekee ambacho watanzania wanakikubali hasa kutokana na kuwa na historia ya kudumisha amani hapa nchini.

“Natambua kuwa vyombo vya habari vimeripoti kuwa Chadema wanatarajia kupata wabunge 70 ambao watahama CCM na kujiunga na Chadema, napenda kuwahakikisha watanzania hususani mwananchi wa mkoa wa Mbeya kwamba mimi siyo mojawapo, nitaendelea kuwa mwaminifu kwa chama changu cha  CCM,” alisema Dk .Mwanjelwa.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles