Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mfumuko wa bei washuka

16th March 2012
Print
Comments

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa vitu mbalimbali umeshuka hadi asilimia 19.4 kwa Februari mwaka huu ukilinganisha na asilimia 19.7 kwa Januari 2012.

Taarifa iliyotolewa jana na  Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), imesema kuwa kupungua kwa mfumuko wa bei wa  Februari 2012 kunamaanisha kuwa, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma imepungua.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa kwa ujumla farihisi za bei zimeongezeka hadi 127.05 kwa Februari 2012 kutoka 106.4, kwa Januari 2011, aidha mfumuko wa bei wa vyakula na vinywaji baridi umepungua hadi asilimia 26.7 kwa Februari 2012, kutoka asilimia 27.8 kwa Januari 2012.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mfumuko wa bei ambao haujumuishi vyakula na nishati kwa Februari 2012 umepungua  hadi asilimia 8.6 kutoka asilimia 9.0 kwa Januari 2012, aidha kwa upande mwingine, mfumuko wa bei wa nishati umeongezeka hadi asilimia 33.5 kwa Februari 2012 kulinganisha asilimia 30.1 kwa Januari 2012.

Aidha taarifa hiyo imesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa nishati kumesababishwa na kuongezeka kwa bei za umeme kwa asilimia 36.7.

Badiliko la farihisi ya bei za bidhaa za vyakula majumbani na migahawani limepungua kwa asilimia 25.5 kwa februari 2012 ikilinganishwa na na asilimia 26.2 kwa januari 2012, aidha kasi ya ongezeko kwa bidhaa zisizo za vyakula imebakia kuwa asilimia 11.8 kwq februari 2012 kama ilivyokuwa kwa Januari, 2012.

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa katika kipindi cha kati ya Februari 2011 hadi Februari 2012, kumekuwa na mwenendo wa kuogezeka  kwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali kutoka asilimia 7.5 kwa 2011 hadi asilimia 19.7 kwa Januari 2012 na kupungua kidogo hadi asilimia 19.4 kwa Februari 2012.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles