Saturday May 25, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Bakwata bado lamng`ang`ania Dk. Ndalichako

7th June 2012
Print
Comments
Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Joyce Ndalichako

Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) limeendelea kumng’ang’ania Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Joyce Ndalichako, likimtaka kujiuzulu ili kulinda heshima ya serikali.

Baraza hilo limesema limepoteza imani na Necta na hivyo kutaka serikali iunde tume huru kuchunguza utendaji kazi wa baraza hilo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa jana, Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti  Issa Shaaban Simba, alisema hatua hiyo inatokana na waislamu nchini kutoridhishwa na matokeo mitihani ya kidato cha sita yaliyotangazwa Mei Mosi mwaka huu  katika somo la elimu ya dini ya Kiislaamu (Islamic knowledge), ambapo  takribani asilimia 70 ya wanafunzi walifeli kwa kupata daraja F.

Mufti Simba alisema katika waliofaulu walipata alama za juu ni asilimia 30 tu ambapo ni wanafunzi saba tu ndio walipata daraja D hatua iliyopelekea  matokeo ya somo hilo kuwa ni la mwisho kwa ufaulu kwa nchi nzima.

“Matokeo haya yaliwashtua wazazi na walimu wa somo hili ambapo waliamua kukata rufaa na ndipo Necta ikaamua kufanya mabadiliko ya matokeo na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa asilimia 70 jambo hili ni kashfa kwa Baraza la Mitihani na serikali kwa ujumla”,alisisitiza kiongozi huyo wa dimi.

Alisema Bakwata inamshangaa, Dk. Ndalichako, kwa kauli yake aliyoitoa Juni 5 mwaka huu kupitia vyombo vya habari kwamba hakuna hujuma na mitihani ilisahihishwa na walimu wenye sifa na waliochaguliwa na wakuu wa shule zao kwa mfumo wa usahihishaji unaoitwa Conveyor Belt.

“Bakwata inasema tatizo sio mitihani kusahihishwa na walimu wenye sifa, tunahoji nani aliwachagua walimu hao na mfumo wa usahihishaji uliotumika tatizo la msingi ni kufelishwa kwa makusudi kwa wanafunzi wa kiislamu katika somo husika wakati nakala za mitihani yao zinaonyesha wamefaulu”, alifafanua Mufti Simba.

Alisema kutokana na hali Bakwata inaitaka serikali kuwawajibisha mara moja watendaji wakuu wa Necta wa kitengo cha mitihani wanaohusika na mfumo wa kompyuta sambamba na kutaka hatua zakisheria na  kinidhamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa baraza hilo watakaothibitika kuhusika na kashfa hiyo.

Mapema wiki hii, Dk. Ndalichako, alikanusha Necta kufanya upendeleo au hujuma kwenye usahihishaji wa mitihani, akisema jambo hilo hufanywa kwa kufauata taratibi na sheria zilizopo.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment