Wednesday Jun 19, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

ADB yaikopesha Tanzania mabilioni ya kujenga barabara

24th May 2012
Print
Comments
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijjah

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha imesaini makubaliano ya mkopo wa Sh. bilioni 354.56 na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kusaidia  ujenzi wa barabara mbalimbali nchini.

Makubaliano hayo yalisainiwa jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijjah, na Mwakilishi wa Benki hiyo nchini, Tonia Kandiero, ambapo ujenzi huo unatarajia kuanza Oktoba mwaka huu na kukamilika mwaka 2017.

Khijjah alisema ujenzi wa barabara hizo utagharimu Sh. bilioni 538.88 ambapo shirika la Misaa la Kimataifa la  Japan (JICA) litatoa msaada wa Sh. bilioni 157.4 na serikali ya Tanzania itachangia Sh. bilioni 27.0.

Khijjah alizitaja barabara zitakazojengwa kuwa ni Dodoma-Babati kilomita 188,Tunduru-Mangaka-Mtambaswala kilomita 202.5 ambapo alisema kukamilika kwa baraba hizo kutasaidia baadhi ya wakulima na wafanyabiasha kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi na kupunguza umaskini.

Aidha, alisema fedha hizo  zitatumika katika kutoa elimu kwa wakandarasi wa kike na kuwalipa fidia wakazi ambao wataathirika kwa nyumba zao kuvunjwa wakati wa ujenzi huo.




 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment