


.jpg)
Rais Jakaya Kikwete ametaka mabadiliko ya utendaji mzuri wa serikali katika kutimiza majukumu yake zikiwa jitihada za kukuza uchumi wa nchi.
Kwa kujibu wa Rais Kikwete, mawaziri wote watatakiwa kupitia mipango yao ya kimkakati kwa kuzingatia vipaumbele kwa muda uliopangwa.
Rais alitoa kauli hiyo jana alipokuwa anafunga warsha ya siku mbili kuhusu Utekelezaji, Ufuatiliaji na Tathmini kuhusu Mpango wa Taifa wa Maendeleo mjini hapa.
Kikwete alisema nchi haifanyi vizuri katika kutambua vipaumbele, kutengeneza mifumo bora, utekelezaji, tathmini na kufuatilia mambo na mambo ambayo yanachangia kuboresha uchumi.
“Tunapaswa kubadili njia zetu za kufanya mambo, kwa kujielekeza na kuwa na malengo Natumaini tunaweza kuyafanya kwa kutumia dira ya mwaka 2025,” alisema.