Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Cirkovic kubomoa safu ya ulinzi Simba

16th May 2012
Print
Comments
Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic

Baada ya timu yake kutolewa nje katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho, kocha wa Simba, Milovan Cirkovic, amesema kuwa amepanga kuisuka upya safu ya ulinzi kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.

Simba ni moja kati ya timu tatu ambazo mwezi ujao zitaiwakilisha Bara katika mashindano ya Kombe la Kagame yatakayofanyika hapa nchini kwa mwaka wa pili mfululizo.

Akizungumza muda mfupi baada ya kurejea nchini, Cirkovic alisema kuwa safu ya ulinzi ilionyesha mapungufu makubwa katika mechi mbalimbali walizocheza hivyo anahitaji kupata nguvu mpya kuimarisha eneo hilo.

Safu ya ulinzi ya Simba inaundwa na Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Amir Maftah, Nassoro Said 'Chollo' na Shomari Kapombe ambao wote wameitwa katika timu ya taifa, Taifa Stars, inayojiandaa kuivaa Ivory Coast katika kuwania akufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika, huku wengine wakiwa ni Mganda Dereck Walulya ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu na veterani Victor Costa, ambaye aliyetuhumiwa kuwa uchochoro nchini Sudan.

Cirkovic huyo alisema ili kuepusha makosa hayo yasijirudie msimu ujao anahitaji pia kupata kiungo mwenye uwezo ambaye atasaidia kutengeneza nafasi za mashambulizi kwenye timu hiyo.

"Yaliyotokea huko ni historia na sasa najipanga kwa ajili ya msimu ujao na mashindano mengine, ndio soka lilivyo, kila siku ni kujifunza na haina mwisho," alisema kocha huyo.

Mserbia huyo alisema pia wachezaji wake walipambana kuhakikisha wanafanya vizuri lakini magoli ya haraka yaliwapunguzia kasi waliyokuwa nayo kwenye kipindi cha kwanza.

Alisema kuwa suala la penati huwa halina ufundi zaidi kwa sababu mara nyingi wachezaji nyota hushindwa kutumia nafasi hizo vizuri lakini hiyo yote ni sehemu ya mchezo.

Nahodha wa Simba, Juma Kaseja, ambaye alikosa penati na kuipa ushindi Al Ahly Shandy, alisema matokeo hayo si mwisho wa kila kitu ila watajipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano ya Klabu Bingwa Afrka msimu ujao.

Kaseja alisema kuwa mechi ilikuwa ngumu pamoja na uchovu wa safari, vilikuwa ni sababu nyingine zilizochangia wao kutochezesha katika kiwango chao cha kawaida.

Wachezaji wa timu hiyo wamepewa mapumziko lakini wenzao 11 jana jioni walitarajia kuungana na wachezaji wengine katika kambi ya timu ya taifa ya soka, Taifa Stars, ambayo inatarajia kuanza mazoezi leo kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi itakayofanyika Mei 26 hapa jijini Dar es Salaam.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles