Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

`TCRA fuatilieni matatizo huduma za simu

24th May 2012
Print
Comments
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia January Makamba

Naibu  Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia January Makamba, ametoa wiki mbili kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzungumza na makampuni ya simu nchini ili yatoe majibu kuhusiana na kuwepo kwa matatizo ya huduma za simu na lini yatatatuliwa.

Makamba alitoa agizo hilo jana alipotembelea ofisi za TCRA kujionea utendaji kazi wake.

Alisema licha ya kukua kwa sekta ya mawasiliano nchini, lakini kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wateja wanaotumia huduma za simu kwamba zinasumbua.

“Ninaongea kama mwananchi wa kawaida ambaye pia ninatumia huduma hii, licha ya kusikia malalamiko kutoka kwa wananchi lakini mimi pia ninatumia huduma ya simu, nimeshuhudia kuwepo kwa matatizo ya mitandao hii,” alisema.

“Unaweza kupiga simu ukaambiwa haipatikani hata kama iko hewani, au ukakatwa fedha nyingi tofauti na matumizi, lakini tatizo lingine ni lile la kutumiwa ujumbe mwingi wa promosheni,” aliongeza.

Makamba alisema haiwezekani makampuni ya simu yakawa yanatumia fedha nyingi katika promosheni pasipo kujali kuweka miundombinu yao vizuri na kuitaka TCRA kuhakikisha matatizo hayo yanashughulikiwa haraka.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles