Monday May 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mnyika ataka mgomo wa madaktari ujadiliwe

2nd July 2012
Print
Comments

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, amemwandikia Spika wa Bunge, Anne Makinda, kutaka aruhusu Bunge kujadili hali ya huduma katika hospitali za umma na jaribio la kutaka kuuawa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka.

Mnyika katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba Kumb: OMU/BJMT/016/2012, ya Juni 30, mwaka huu, anasema hatua hiyo italiwezesha Bunge kutumia madaraka yake kwa mujibu wa Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya nchi kuisimamia serikali kuokoa uhai wa wagonjwa na kuishauri kushughulikia chanzo cha mgogoro kati yake na madaktari.

Hivyo, amemuomba Spika kutoa idhini kwa mujibu wa kanuni ya 150 (1) ya kutolewa kwa hoja ya kutengua kanuni ya 64 (1) (c) ya Bunge kuliwezesha Bunge kujadili Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii.

Mnyika alisema Spika anaweza kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kanuni 114 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge kutaka kamati husika ya Bunge kukutana kwa dharura na kuishauri kwa haraka serikali kufuta kesi iliyoko Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi.

Au kutafuta suluhu ya nje ya mahakama ili kulipa fursa Bunge kutumia madaraka yake ya kikatiba kujadili na kupitisha maazimio ya kusuluhisha pande mbili za mgogoro badala ya mahakama ambayo mchakato wake utachukua muda mrefu kukamilika huku wananchi wakiendelea kuathirika.

“Uamuzi wa kurejea mahakamani unapaswa kuwa wa mwisho baada ya hatua zingine kushindikana,” alisema.

Alisema pia Spika kwa kutumia mamlaka yake kwa mujibu wa kanuni ya 114 (17)  na 116 anaweza kuitaka Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kupatiwa na kupitia nyaraka zilizowasilishwa mahakamani.

Pia kuandaa taarifa maalum ya masuala yanayoweza kujadiliwa bungeni bila kuingilia suala lililo mahakamani.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment