Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Benki ya Vijana ya CCM kuanzishwa

12th May 2012
Print
Comments
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Martin Shigela

Benki ya  Taifa ya Vijana  inatarajiwa kuzinduliwa wakati wowote mwaka huu.

Uzinduzi utafanyika baada ya mchakato wa kufunguliwa kwa benki ya vijana ya taifa kuingia katika hatua za mwisho, Katibu Mkuu wa Umoja wa  Vijana wa  CCM –(UVCCM) Taifa, Martin Shigela amesema.

Alisema hayo wakati akizindua kikundi cha wajasiliamali wa umoja huo katika kata ya Manyoni mkoani Singida.

Alifahamisha kuwa mchakato  wa kuanzishwa benki hiyo kupata usajili wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Alisisitiza kuwa taasisi hiyo itawezesha wajasiriamali wa kati na wadogo yakiwemo makundi ya wanawake kujikwamua kiuchumi.

Aliongeza kuwa ni  azma ya serikali ya CCM  ya kuwawezesha vijana  hasa kuwapatia mtaji. Alisema tayari UVCCM ngazi ya taifa imefanya mazungumzo na mifuko ya hifadhi ya Jamii pamoja na taasisi nyingine za fedha ambazo zimeonyesha nia ya kusaidia vijana wakiwemo waendesha  boda boda na vikundi vingine..

Awali akisoma risala ya kikundi hicho cha wajasiriamali, Katibu Uhamasishaji wa Kikundi Bahati Matonya alisema kikundi hicho kinakabiliwa na changamoto ya vitendea kazi zikiwemo zana za kilimo.

Alisema hali hiyo inakwamishwa maendeleo ya shamba la kikundi lenye hekari  zaidi ya 200 na kumuomba Katibu Shigela kusaidia kupata wafadhili.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles