Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Polisi wazuia Nchunga asitupwe nje klabuni

12th May 2012
Print
Comments
Gari la polisi walioitwa na mwenyekiti Lloyd Nchunga likiwa nje ya klabu ya Yanga jana asubuhi baada ya kutokea mabishano makali baina ya pande mbili za wanachama, kila moja ikipinga uongozi ama kundi la vijana kufanya mkutano mahala hapo. (Picha fullshangwe.blogspot.com)

Mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga jana alifanikiwa kuzungumza na waandishi wa habari kwa kukingiwa kifua na jeshi la polisi baada ya wanachama wanaotaka ajiuzulu mara moja kutaka kuingia klabuni kumchomoa.

Hali hiyo ilifuatia wanachama wa Yanga wanaomuunga mkono na wanaoshinikiza ajiuzulu chini ya Bakili Makele kuonyeshana ubabe nje ya klabu hiyo.

Hali hiyo ya vurugu ilikuja kutulizwa na askari polisi baada ya magari mawili ya jeshi hilo kufika klabuni hapo kwa lengo la kulinda amani.

Ili kuondoa hali ya uvunjifu wa amani klabuni hapo, polisi ilifanya mkutano na pande mbili za vijana wanaoongozwa na Bakili pamoja na uongozi wa klabu hiyo.

Baada ya mkutano huo, polisi iliwataka wanachama wa klabu hiyo pamoja na waandishi wa habari kutawanyika kwa kuwa hakuna mkutano ambao ungefanyika.

Lakini wakati wanachama wanatawanyika, Nchunga ambaye muda wote hakuonekana nje alijitokeza na kuwaita waandishi wa habari na kuanza kuzungumza nao hali iliyosababisha kundi la Bakili kulalamika juu ya mkutano huo.

Wakati Nchunga akizungumza na wanahabari, mlangoni walikaa askari wa jeshi la polisi pamoja na baadhi ya wanachama wanaomuunga mkono kulinda wanachama wengine wasiingie na kuleta vurugu.

Vurugu hizo zilitokea klabuni hapo asubuhi baada ya wanachama kuanza kujikusanya kufuatia kuwepo kwa taarifa ya kufanyika kwa mkutano wa vijana wa klabu hiyo ambao wanashinikiza Nchunga ajiuzulu.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa klabu naye alikuwa ameitisha mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kuelezea mambo ya klabu hiyo mahala hapo pia.

Mkutano huo wa Nchunga na Wanahabari uliokuwa umepwangwa kuanza saa 5:30 asubuhi ulichelewa kuanza kwa zaidi ya masaa mawili kutokana na vurugu hizo za wanachama.

Kundi moja linalomuunga mkono Nchunga lilikuwa likiwasisitizia wenzao wanaotaka Nchunga ajizulu kuwa mwenyekiti huyo hawezi kufanya hivyo kwa matakwa yao na badala yake waliwataka wasubiri mkutano mkuu ndipo wapeleka hoja hiyo.

"Nchunga amewekwa madarakani na wanachama kwenye uchaguzi wa halali sasa kama nyinyi mtanaka ajiuzulu fuateni tataribu kwa kusubiri siku ya mkutano mkuu ndipo muleta hoja zenu lakini kwa sasa hivi huyo ni mwenyekiti wetu halali," alisema Hamis Said mwanachama wa klabu hiyo mwenye kadi namba 024.

Hata hivyo kundi lingine ambalo linaongozwa na Bakili Makele liliendelea kupiga kelele kusisitiza Nchunga ajiuzulu kwa kuwa ameshindwa kuingoza.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles