Wednesday May 4, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Twiga Stars yaumizwa 5-2

21st May 2012
Print
Comments
Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars

Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Afrika Kusini, Banyana Banyana, iliendeleza ubabe kila inapokutana na timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, wakati ilipowashushia kipigo kizito cha mabao 5-2 katika mechi yao ya kirafiki ya kujiandaa na mechi za kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. 

Twiga itacheza mechi yake ya kufuzu dhidi ya Ethiopia mjini Addis Ababa Mei 26, wakati Banyana itakuwa ugenini Zambia siku hiyo hiyo. 

Katika mechi ya jana, Banyana walipata goli la kwanza katika dakika ya 23 kupitia kwa Patricia Modise aliyeuwahi mpira uliorudishwa nyuma na beki wa Twiga, Mwanaidi Tamba, na kufanya matokeo ya 1-0 yaliyodumu hadi wakati wa mapumziko.

Modise tena akaipatia Banyana goli la pili kwa kichwa kufuatia krosi ya Gabisile Hlumbane, Fatuma Bushiri aliifungia Twiga Stars goli la kwanza kwa njia penalti iliyotolewa na mwamuzi wa FIFA, Judith Gamba, baada ya Mwanahamis Omary 'Gaucho' kuangushwa na Janine van Wyk ndani ya boksi katika dakika ya 63.

Wageni walipata goli la tatu katika dakika ya 73 kupitia kwa Sanah Mollo aliyeingia kuchukua nafasi ya Andiswe Mgloyi baada ya mabeki wa Twiga kujichanganya.

Asha Rashid 'Mwalala' alifanya matokeo yawe 3-2 katika dakika ya 77 kufuatia pasi ya Fatuma Mustapha, lakini dakika mbili baadaye Banyana walipata goli la nne lililofungwa na Sanah tena.

Na dakika nne kabla ya mechi kumalizika beki Janine van Wyk aliwafungia Banyana goli la tano kwa mpira wa 'fri-kiki' iliyokwenda moja kwa moja wavuni. Mara ya mwisho wakati timu hizo zilipokutana katika fainali za Mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusuni, Twiga ililala 2-1. 

Kikosi cha Twiga Stars jana kilikuwa: Fatuma Omary, Fatuma Khatibu, Mwajuma Abdallah, Fatuma Bushiri, Mwanaidi Tamba, Everine Sekikobo, Esther Chabruma 'Lunyamila', Mwanahamisi Omary 'Gaucho', Asha Rashid 'Mwalala', Mwapewa Mtumwa na Fatuma Mustapha.

Banyana: Roxanne Barker, Nodhano Vilakazi, Amanda Sister, Janine van Wyk, Zamandosi Cele, Amanda Dlamini, Mary Ntsweg, Patricia Modise, Gabisile Hlumbane, Rafilde Jane, Andiswe Mgloyi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles