Thursday May 23, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Wabunge wakataa bajeti ya Wizara

9th June 2012
Print
Comments
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mtaa (LAAC), Idd Azzan,

Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wamegoma kupitisha bajeti ya Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana kwa kuwa imeshindwa kutoa mchanganua wa bajeti ya mwaka uliopita.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jenista Muhagama, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi kuhusu suala hilo ambapo alisema kuwa wameshindwa kuipitisha bajeti ya wizara hiyo kwa kuwa haijaonyesha kiasi cha fedha ilichopewa na matumizi yake.

Alisema wizara hiyo ilitakiwa kutoa ufafanuzi sahihi kuhusu bajeti iliyopita ili Kamati iweze kuipitisha lakini imeshindwa kufanya hivyo.

Muhagama alisema waliipatia muda wa  kuonyesha ripoti ya mchanganua wa bajeti iliyopita na kwamba matumizi ya miradi ya maendeleo hazikuwekwa, hivyo Kamati haikuwa tayari kuipitisha bajeti hiyo.

Wakati huo huo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Murtaza Magungu (CCM), ameitaka serikali kuipatia Bodi ya Mazao Mchanganyiko na Nafaka kiasi cha Sh bilioni 10 kama mtaji ili waweze kuingia katika ushindani wa biashara kwa lengo la kushusha gharama za vyakula.

Alisema bodi hiyo itakuwa inafanya kazi yake ya kununua chakula kwa wakulima na kuviuza kwa wananchi kwa gharama nafuu ili kushindana na wafanyabiashara katika kushusha bei za vyakula.

Magungu alisema endapo serikali ikishindwa kuweka ushindani katika biashara tatizo la mfumuko wa bei litaendelea kuwakabili wananchi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za  Mtaa ( LAAC), Idd Azzan, ameagiza Mkaguzi wa Ndani wa Hesabu za Halimashauri ya Wilaya ya Nkasi kukatwa asilimia 15 ya mshahara wake wa mwezi huu kutokana na uzembe aliouonyesha.

Alisema hakuna mchanganuo wa fedha dhidi ya miradi mbalimbali iliyofanyika katika Halmashauri hiyo ambapo ilitakiwa ikaguliwe mahesabu yake.

"Hatutaki kuona figure tunahitaji kuona huo mchanganuo wa matumizi ya fedha yalivyofanyika ikifika Julai 8, muwe mmeshatupatia matumizi ya miradi hiyo kwani mahesabu yenu yana mikanganyiko," alisema.

Alisema Mkaguzi wa ndani anatakiwa kulisimamia suala hilo kwa umakini na kujua mchanganua ya fedha hizo za miradi zilivyotumika hivyo adhabu hiyo itamfanya asimamie shughuli zake kwa umakini.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment