Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

RC aunda timu ya mgogoro Arumeru

24th April 2012
Print
Comments
  Vijana wafanya vurugu kubwa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo

Timu ya wataalamu watano ambayo imeundwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, kushughulikia mgogoro kati ya wanavijiji na mwekezaji  wa kigeni anayemiliki shamba la Dolly, wilayani Arumeru, inaanza kazi leo.

Mulongo alisema hayo baada ya mazungumzo yake na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa iliyokutana kuzungumzia hali ya ulinzi na usalama mkoani hapa.

Bila kutaja majina ya wajumbe wengine waliomo kwenye timu hiyo, Mulongo alisema itaongozwa na Mkuu wa Idara ya Miundombinu mkoani hapo, Jackson Ole Saibatahu. Alisema timu hiyo itafanya kazi kwa wiki moja kuanzia inatarajiwa kumaliza kazi yake baada ya wiki moja kuanzia leo.

Baadhi ya wavijiji wa Kitefu, Migadini, Maroroni na Ugoro katika kata hizo mbili, walivamia shamba la Dolly linalom ilikiwa Jerome Bruins na kufanya uharibifu wa miundombinu ambapo walivunja fensi ya umeme yenye urefu wa miza 2000 pamoja na kuchoma moto vibanda vya walinzi. Baada ya uharibifu huo, wakazi hao waliingiza makundi ya mifugo katika shamba hilo kwa ajili ya malisho.

Wakati mgogoro huo ukiendelea, mamia ya wakazi  wengine kutoka maeneo ya Nduruma, Nkoanrua na Akheri wilayani humo, walivamia shamba linalomilikiwa na kampuni ya Machumba na kugawana maeneo kwa madai kuwa hawana ardhi ya kuzalisha chakula kwa ajili ya familia zao.

Mulongo alisema madai ya kutaka kurejeshewa ardhi yao ni madai ambayo yanapaswa kushughulikiwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa kisheria. Alisema serikali ya mkoa haitasita kuchukua hatua kwa mtu ye yote atakayeendelea kujihusisha na vitendo hivyo kwa uvunjaji wa sheria.

Wakati serikali ikijaribu kutafuta mwafaka, kundi la vijana kutoka katika eneo la Ambreni jana lilifunga barabara ya Arusha-Moshi kwa mawe na magogo.Tukio hilo lilidumu kwa saa mbili na kusababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wakitoka katika miji ya Arusha na Moshi.

Wananchi hao wengi wakiwa vijana walikuwa wakipiga kelele wakisema kuwa wagawiwe mashamba hayo kwani wanakabiliwa na umasikini kutokana na kutokuwa na kazi za kufanya. Polisi walipambana nao kwa saa mbili na hatimaye kuifungua barabara hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa.

“Hivi ni vitendo vya kihuni, juzi tulikwisha zungumza na wananchi hao na serikali ikakutana nao na madai yao yanafanyiwa kazi, hatuko tayari kuvumilia vitendo vya aina hii,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mercy Silla alisema kuwa tayari kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya imeshakutana na wananchi ambao walitoa madai yao na yanashughulikiwa.

“Walisema wanataka kujenga shule hawana eneo na tumeongea na mmiliki wa shamba la Machumba, akasema kuwa ni suala linalozungumzika, pia walisema kuwa miti aina ya mikaratusi imepandwa katika chanzo cha maji hilo nalo mmiliki alikubali kulitizama,” alisema Silla.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles