Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

UVCCM Arusha sasa ni vurugu tupu

26th April 2012
Print
Comments

Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Arusha, (UVCCM), wamefunga ofisi ya makao makuu ya umoja huo mkoani hapa na kubandika mabango yaliyokuwa yakishutumu hatua ya Katibu wa UVCCM mkoa, Abdallah Mpokwa kumsafisha aliyekuwa mwenyekiti wa umoja huo, James Ole Millya.

Imeelezwa kuwa ofisi hizo zilizopo eneo la Kaloleni zilifungwa majira ya usiku wa kuamkia jana na watu wasiojulikana na hadi sasa hazijafunguliwa.

Baada ya kujitoa CCM hivi karibuni, Millya alihamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), lakini baadhi ya vijana hao wanamtuhumu kwa ufisadi.

Baadhi ya vijana wa umoja huo, Ally Shaaban maarufu kwa jina la Majeshi ambaye ni Katibu wa UVCCM

Kata ya Moshono pamoja na Masoud Rajabu ambaye ni

Katibu wa UVCCM, Kata ya Lemara, walisema wamechukizwa na kauli ya

Mpokwa aliyoitoa juzi kumsafisha Millya kwa madai hana ushahidi wa Sh. milioni mbili iliyotolewa kwa ajili ya kuanzishwa kwa Chama cha Kuweka na Kukopa (Saccos) cha umoja huo.

Shaaban alihoji ni kwa nini Mpokwa amtetee Millya kuhusu suala la fedha na mambo mengine hivyo uamuzi wa vijana kufunga ofisi hiyo ni sahihi kwani tamko alilolitoa halina mashiko na kama vijana hawamtaki tena kuongoza umoja huo.

Naye Rajab aliongeza kuwa wanamhitaji mlezi wa chama hicho mkoani hapa, Steven Wassira, aende kurekebisha matatizo ya umoja huo.

Baadhi ya vijana wa umoja huo walionekana wakiwa makundi makundi kila mmoja akimvizia mwenzie kuona ni nani atavunja ofisi hiyo huku wengine wakidai mtu akisogea kufungua makufuli hayo waliyoweka watahakikisha wanapigana na kusisitiza Mpokwa aondoke kwani hawamhitaji tena.

NIPASHE ilimtafuta Mpokwa, lakini wakati wote siku yake ilikuwa inatumika.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles