Wednesday Jun 19, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

APR, URA, AS Vita kuwasili leo

12th July 2012
Print
Comments
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Rwanda, APR na klabu za URA ya Uganda na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinatarajiwa kuwasili nchini leo kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) ambayo yanatarajiwa kufanyika nchini kuanzia keshokutwa Jumamosi.

Yanga ambao ndio mabingwa watetezi wa mashindano hayo, watafungua dimba kwa kucheza dhidi ya Atletico ya Burundi kuanzia saa 10:00 jioni huku mechi ya mchana ikiwa ni kati ya APR na Wau Salaam kutoka Sudan Kusini.

Akizungumza jana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa timu hizo zinatarajia kuwasili kwa nyakati tofauti, lakini maandalizi yao ya malazi na mapokezi yameshafanyiwa kazi. Atletico na Wau Salaam zilitarajiwa kuwasili jana usiku.

Wambura alisema kuwa kila timu inatarajiwa kuja na msafara wa watu 25 na leo ndio mwisho wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kupokea majina ya wachezaji watakaozitumikia timu zilizothibitisha kushiriki mashindano ya mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Wambura alisema kuwa leo, waamuzi mbalimbali kutoka nchi wanachama walioteuliwa kuchezesha michuano hiyo watashiriki katika mtihani wa waamuzi, zoezi ambalo hufanyika kila mwaka kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

Hadi sasa, mlezi wa CECAFA, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ndiye mdhamini pekee aliyethibitisha kusaidia michuano hiyo kwa kutoa fedha kwa ajili ya zawadi ambayo ni dola za Marekani 60,000 (Sh. Milioni 90).

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment