Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Circovik akiri Shandy ngumu

28th April 2012
Print
Comments
Kocha wa klabu ya Simba, Mserbia Milovan Cirkovic

Kocha wa klabu ya Simba, Mserbia Milovan Cirkovic amesema kuwa ameiona timu ya Al-Ahly Shandy kupitia video za michezo yake na kusema mchezo wa kesho baina yao utakuwa mgumu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Milovan alisema Al-Ahly Shandy ni timu nzuri na wanategemea upinzani mkubwa kwenye mchezo wao wa kesho wa raundi ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika.

"Kwa jinsi nilivyowaona ni timu nzuri ambayo itatoa upinzani na kuufanya mchezo kutokuwa mwepesi lakini tumejipanga kukabiliana nao," alisema Milovan.

"Mchezo wa mpira hutakiwi kudharau timu yoyote, lengo letu sisi ni kuhakikisha tunasonga mbele kwenye mashindano haya na hilo wachezaji wanalitambua.

"Tumejiandaa vizuri kukabiliana nao."
Milovan alisema anashukuru timu yake haina majeruhi na hivyo atakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi kwenye mchezo huo.
Alisema Shomari Kampombe ambaye alitolewa baada ya kuumia kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Moro United anaendelea vizuri na anaweza akawemo kwenye kikosi kitakachowavaa wasudan hao.

Kwa upande wake, Akizungumza baada ya mazoezi ya timu hiyo jana kwenye uwanja wa Karume, Kocha wa Al-Ahly Shandy, Mohammed Kouk alisema kuwa mchezo wa kesho utakuwa mgumu kwao kwa kuwa wanapambana na timu kubwa na yenye zoefu wa mashindano ya Kimataifa.

Alisema kuwa anaifahamu Simba na anajua ni timu kubwa hivyo watacheza kwa tahadhari kwenye mchezo wa kesho ili kupata matokeo mazuri.

"Tunajua ugumu wa mchezo wetu na Simba... ni timu nzuri na yenye uzoefu mkubwa kuliko sisi lakini soka haliangalii hilo," alisema.

"Tutacheza kwa umakini mkubwa ili tupate matokeo mazuri yatakayoturahisishia kazi kwenye mchezo wa marudiano kule kwetu."

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles