Sunday May 26, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mrithi wa Kim U-20 alonga

27th June 2012
Print
Comments
Kocha mpya wa timu ya soka ya vijana ya umri chini ya miaka 17 na 20, Jakob Michelsen

Kocha mpya wa timu ya soka ya vijana ya umri chini ya miaka 17 na 20, Jakob Michelsen, kutoka Denmark, amesema kuwa falsafa yake ni kuona timu anayoiongoza inakuwa na wachezaji wanaochezea zaidi mpira kwa lengo la kushambulia.

Michelsen alisema hayo wakati akitambulishwa ramsi na uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) jana ambao ulitangaza kumpa mkataba wa mwaka mmoja.

Michelsen alisema kwamba anaamini mfumo huo wa uchezaji utasaidia kukuza vipaji vya nyota hao chipukizi na hapendelei mfumo wa kuzuia kama baadhi ya makocha wengine wanavyofanya.

"Falsafa yangu ni kuona wachezaji wanakuwa na uwezo wa kumiliki na kushambulia muda wote wa mchezo na huu ndio mfumo utakaosaidia wachezaji chipukizi kujifunza zaidi na kuona uwezo wao badala ya kujipanfa kuzuia, iwe ugenini au nyumbani," alisema kocha huyo ambaye alipendekezwa na Kim Poulsen, ambaye kwa sasa anaiongoza timu ya Tanzania (Taifa Stars).

Kabla ya kuja Tanzania, Michelsen alikuwa kocha wa timu ya daraja la kwanza ya Hobro IK ya Denmark na ana leseni A ya ukocha kutoka Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA), leseni ya ukocha wa vijana kutoka Chama cha Soka la Denmark (DBU).
Moja ya mafanikio yake ni kuipa ubingwa wa Denmark, timu ya Skovbakken kwenye ligi ya timu zenye umri chini ya miaka 18. Ubingwa huo aliupata msimu wa 2005/2006.

Kocha huyo tayari ameshuhudia timu nane kati ya 12 zinazoshiriki mashindano ya UMISETA huko Kibaha na baadhi ya mechi za michuano ya Copa Coca Cola inayoendelea.

Naye Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, jana alisema kuwa ili kudhibiti vijeba shirikisho limepanga kutumia kipimo cha MRI ili kuhakikisha umri wa wachezaji kabla ya kuanza kwa maandalizi ya kuivaa timu ya vijana ya Kenya katika mchezo wao wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za vijana za Afrika.

 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment