Friday May 24, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Mambo muhimu 10 mtoto afundishwe

27th March 2012
Print
Comments

Mambo  10 ya jumla jumla ninayodhani ni muhimu kumfundisha mwanao na siku za usoni nitaendelea na mambo maalum (specific) kama nilivyofanya wiki iliyopita.

 Kabla ya kuyataja hayo 10, ninaomba nisisitize kwamba wazazi tuchunge umri wa kuanzia miaka minne hadi 10 katika kuwafundisha wanetu. Wengi utasikia wanasema “katika umri huu mtoto atajifunza nini” wakidhani watamfundisha akishakua mkubwa kidogo ya hapo, lakini wataalamu wengi wa masuala ya saikolojia wanaonyesha kwamba huo ndio wakati mwafaka wa kumfundisha mwanao mambo yote ya msingi kuhusu maisha na ukiupoteza, akajifunza mambo ya hovyo basi ujue, ‘imekula kwako’.

Jambo la kwanza la kumfunza mwanao ni kumwambia kila wakati asubiri hadi anayeongea amalize kuongea ndipo na yeye aseme ama kujibu anachotaka kujibu. Yaani asimwingilie kati mtu anayeongea.

Mtoto ajifunze kwamba hakuna atakayesikika kama kila mmoja anaongea kwa wakati mmoja. Ajue kwamba hata kama ana swali ahakikishe anauliza pale panapokuwa hakuna anayeongea.

Hata wewe mzazi jenga mazoea ya kutomkata kauli mwanao anapokuwa anaongea ama kujitetea (pale anapokuwa kafanya makosa). Hii pia itamsaidia kujenga tabia ya kusubiri mtu amalize kusema ndipo na yeye afungue mdomo wake.

 Pili, wazuie watoto tabia ya kupachikana majina hata kama jina hilo linaonekana la kuvutia/kuchekesha. Na wewe pia usithubutu kumpachika majina mwanao ama kumwita mbwa, paka na kadhalika. Tabia ya kupachikana majina inawaumiza wengine.

Badala ya kumpachika mwenzao jina, fanya watoto wapende kueleza tabia ama matendo ya mwenzao yenye kuudhi.

Tatu, watoto wafundishwe kusalimia kila wanapomuona mkubwa. Wafundishwe pia, kusalimia kwa kushikana mikono kutegemea na mazingira, na kwamba hilo si lazima kulifanya kwa watoto wenzao. (Kwa watoto wa Kiislamu wafundishwe  kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono kama wako jinsia tofauti kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao).

Mfundishe mtoto kuwa mchangamfu na kutabasamu mnapotembelewa na mgeni na apende kuwaambia wageni maneno ‘karibu’, ‘karibu kiti’.

Nne, maneno "tafadhali" na "asante" yawe na umuhimu wa pekee kwa mtoto na hakikisha kila mara anayatumia. Maneno hayo yanaonyesha heshima na shukrani. Na kama naye kashukuriwa ajifunze kusema “asante kushukuru”.

Watoto wajifunze kuoga, kunawa kabla ya kula, kujitawadha kwa maji na kunawa na sabuni pamoja na kufagia maeneo yao. Bila kujali jinsia, wafundishwe kufagia nyumba, kudeki, kufua na kuosha vyombo.

Wajifunze pia kupika. Wakichafua ama kuacha takataka mahala, hata kama walikuwa wanacheza, wafundishwe kuziondoa na si kuziacha mahala hapo. Kikubwa wajifunze kusafisha mahala kabla ya kuanzia jambo lingine. Suala la usafi kwa watoto ni muhimu sana na liwe la kila siku.

 Sita, watoto kwenye michezo wafundishwe kujua kuna kushinda na kushindwa. Wanaposhindwa mchezo wajifunze kumpongeza mshindi na anayeshinda ajifunze kwamba ni mwiko kumzomea aliyeshindwa bali ni kumpa moyo kwamba kuna siku naye atashinda.

Nadhani uchache wetu wa kuwafundisha wanetu mambo haya ndio maana tunashuhudia mambo ya hovyo zinapocheza Simba na Yanga. Utamaduni huu ni wa siku nyingi kwa wenzetu Wazungu na mimi nadhani kwamba ni muhimu kuuiga.

 Saba, kadri utakavyokuwa unawapongeza watoto wanapofanya jema ndipo na wenyewe watajifunza kuwapongeza wengine wanapofanya mambo mazuri.

Jambo la nane ni kuwafundisha watoto kuwafungulia mlango wengine, husuan kwa watoto wa mijini. Upo utamaduni wa kizungu ambapo mtu anapokuwa kafungua mlango kuingia kisha akamuona mwingine anakuja, anabaki kaushikilia ili apite kwanza badala ya kuachia/ kuufunga mbele ya uso wake. 

Huu ni utamaduni mzuri wa kuiga hasa kutokana na maisha ya kisasa ya siku hizi. Na mtu anaposhikilia mlango kwa ajili ya watoto ili wapite ndipo afunge nao wajifunze kumshukuru kwa kusema ‘asante’ wakati wanapita.

Watoto wafundishwe kwamba wanapokuwa wanatoka ndani ya jengo waache kwanza wakubwa watoke/wapite na wao wafuate nyuma. Makanisani na misikitini wapende kukaa nyuma na si mbele mbele.

Jambo la tisa ingawa ni gumu kulifundisha lakini ni muhimu na hili ni watoto kuridhika na chochote wanachopewa/kupata, iwe chakula ama nguo isipokuwa maksi ndogo darasani.

 Jambo la tisa kumfuza mwanao ni kuheshimu anapomuona mtu anafanya jambo ambalo ni tofauti na alivyozoea kutegemea mila, dini, ama utaifa wa mhusika. Yaani ajue kwamba ziko tofauti za kutenda jambo lile lile na zote ni sawa na zina maana kutegemea asili, dini ama utamaduni wa mtu husika.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment