Tuesday May 21, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Rais Kikwete aomboleza kifo cha Askofu Mgweno

1st August 2012
Print
Comments
Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Kanisa la ELIM Pentekoste Tanzania, Askofu Peter Liyema Konki, kuomboleza kifo cha aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Marehemu Ayoub Enzi Mgweno kilichotokea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Julai 29 mwaka huu kutokana na ugonjwa wa saratani.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete amesema amesikitishwa na kuhuzunishwa kutokana na taarifa za kifo cha Mtumishi wa Mungu, Askofu Mgweno.

 “Ninatambua kwamba hata baada ya utumishi wake wa kuwachunga vyema Kondoo wa Bwana, Marehemu Askofu Ayoub, enzi za uhai wake, aliendelea kuwa Mtumishi wa Kanisa la ELIM Pentekoste Tanzania kama Mchungaji, hivyo ni dhahiri kwamba kifo chake kimeacha pengo kubwa kwa waumini wa kanisa hilo popote walipo” alisema Rais Kikwete katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari. 

Katika maisha ya utumishi wake, Askofu Ayoub Enzi Mgweno aliwatumikia waumini wa Chalinze na baadaye Tanga kabla ya kustaafu mwaka 2002 akiwa na cheo cha Askofu.  Marehemu pia aliwahi kulitumikia kanisa lake kwa cheo cha Mwenyekiti wa Makanisa ya ELIM Jimbo la Afrika Mashariki na Kati, na ni miongoni mwa waasisi wa Kanisa hilo hapa nchini.




 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment