Monday May 2, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Simba yaanza kutafuta Bil.1/- za CAF leo

29th April 2012
Print
Comments

Simba itahitaji kupata matokeo yatayoiweka katika nafasi nzuri ya kuitoa Al-Ahly Shandy ya Sudan baada ya michezo miwili ya hatua ya 16 bora, ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwania zawadi ya sh. bilioni 1 ya bingwa wa Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika, kwenye Uwanja wa Taifa leo.

Kocha wa Simba Milovan Cirkovic alisema jana timu yake imejipanga kushinda mchezo huo wa nyumbani ili kutengeneza mazingira mazuri ya kusonga mbele baada ya mchezo wa marudiano utakaochezwa jijini Khartoum wiki mbili baadae.

"Kama kocha siwezi kuahidi mashabiki ushindi... mpira una matokeo ya ajabu lakini ninachoweza kusema ni kwamba tumejiandaa kucheza vizuri kwa ajili ya ushindi ila tutaingia uwanjani kwa tahadhari," alisema Milovan.

Na inabidi maana endapo Simba itaingia robo-fainali ya Kombe la Shirikisho itakuwa imejihakikishia kupata zawadi ya sh. milioni 240 endapo itashika mkia kwenye kundi la timu nne.

Lakini habari njema ni kuwa Wekundu wa Msimbazi wanaweza kuamka matajiri endapo watafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ambayo ilifika fainali mwaka 1993 wakati ikiwa Kombe la CAF.

Bingwa wa Kombe la Shikirikisho huzawadiwa sh. bilioni 1 katika dola za Marekani, sh. milioni 691 endapo timu itafungwa katika fainali na hupata sh. milioni 382.4 kama itashika nafasi ya tatu kwenye kundi lake la hatua ya robo-fainali ambayo kizingiti cha kufuzu kwake ni Al-Ahly.

Milovan alisema wataingia uwanjani kwa tahadhari kwa kuwa Shandy wanaonekana kuwa timu nzuri na ambayo imejipanga katika mashindano haya.

Aidha, alisema kuwa anashukuru mpaka kufikia jana hakuwa na mchezaji majeruhi kwenye kikosi chake huku akisema Shomari Kapombe aliyeumia kwenye mchezo wao wa ligi kuu ya Bara dhidi ya moro United, atakuwepo kwenye kikosi kesho.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles