


.jpg)
Sakata la wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania na Zambia (Tazara) limechukuwa sura nyingine baada ya Serikali kugoma kuwalipa mishahara kwa maelezo kuwa shirika linatakiwa kujiendesha lenyewe.
Awali Chama cha wafanyakazi wa Reli (Trawu) kilitoa tamko na kuipa Serikali siku tano kuwalipa wafanyakazi mishahara kutokana na uongozi wa Tazara kushindwa kutekeleza ahadi ya kuwalipa ulioitoa mbele ya aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu.
Akitoa majibu kwenye mkutano uliohudhuriwa na mamia ya wafanyakazi wa Tazara mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa Trawu, Erasto Kihwele, alisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omar Chambo, aliwajibu kuwa Serikali haina fedha za kuwalipa.
Kihwele aliongeza kuwa Serikali inawasihi wafanyakazi wote wa Shirika hilo kufanyakazi kwa bidii ili mishahara yao iweze kupatikana.