Sunday May 1, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Leticia Nyerere akanusha kukamatwa

22nd May 2012
Print
Comments
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Leticia Nyerere

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Leticia Nyerere, amekanusha taarifa zilizotolewa kwenye mtandao mmjoa wa kijamii kuwa amekamatwa na uhamiaji nchini Marekani kwa kosa la kukiuka masharti ya Green Card.

Taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa taarifa zilizotolewa zilikuwa na lengo la kumshambulia na kumharibia jina lake kwa lengo la kuwatia hofu wananchi wa Tanzania waishio Marekani na Tanzania.

Nyerere alisema ameshatoa taarifa hizo kwenye vyombo vya usalama vya nchini Marekani na kwamba upelelezi unaendelea.

Mei 14 mwaka huu, mtandao wa huo ulichapisha makala iliyohusu kukamatwa kwa Mbunge huyo huko Washington DC, Marekani kwa kosa la kukiuka masharti ya Green Card.


SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles