Thursday Jun 20, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

UDSM yaandaa tamasha la utalii

3rd August 2012
Print
Comments
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Masomo ya Shule ya Biashara (UDBS) kwa kushirikiana na wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali duniani, wameandaa kongamano la kimataifa ili kujadili maendeleo ya utalii katika nchi zinazoendelea.

Dk. John Philemon, Mhadhiri katika Idara ya masoko, ambaye pia ni mratibu wa kongamano hilo, alisema kongamano hilo litakalofanyika Agosti 8 hadi 9, 2010 huko Zanzibar litafunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.

Alisema licha ya sekta ya utalii kuwa na mchango mkubwa katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa nchi, bado haijafanikiwa kupunguza umaskini katika nchi zinazoendelea, hivyo kongamano hilo litasaidia katika kupata ufumbuzi wake.

Kongamano hilo la siku mbili litashirikisha wajumbe kutoka nchi 17 duniani ikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya, Botswana, Israel, Nigeria, India, Korea Kusini, Iran na Mexico, Sweden, Uingereza, Namibia, New Zealand, Afrika ya Kusini, Amerika na Ujerumani pamoja na wadau wengine wa utalii kama vile wanazuoni, wajasiriamali na watunga sera.


 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment