Friday May 6, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

`TBS idhibiti bidha zisizo na ubora`

25th April 2012
Print
Comments
Shirika la Viwango Tanzanania (TBS)

Shirika la Viwango Tanzanania (TBS) limetakiwa kupiga marufuku uingizaji bidhaa zisizo na ubora ili kuleta maendeleo na ushindani wa kimasoko kwa wajasiliamali wa ndani pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara ili kulinda  kulinda afya, usalama na mazingira ya mlaji.

Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wajasiriamali wa vikundi vya Jua Kali na Nguvu Kazi Partners katika semina iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam iliyoratibiwa na TBS.

Baadhi ya washiriki walilitaka shirika hilo kuwa na utamaduni endelevu wa kukagua biadhaa zilizokuwa sokoni licha ya kuweka mikakatia chanya ya kuthibiti ubora kabla bidhaa kuingia nchini.

“Licha ya uingizaji bidhaa kwa njia halali zipo njia nyingi haramu ambazo kimsingi TBS wanatakiwa kuzifikia ili kunusuru hali mbaya iliyokithiri kwa bidhaa feki nchini maarufu Mchina jambo ambalo linazorotesha ustawi mzuri wa taifa letu kwa Nyanja ya kimaendelewo na uchumi,” alisema Mama Mzirai mjasiriamali na mchuuzi wa mabegi.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles