Friday Apr 29, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Serikali yajipanga kuongeza wataalam sekta ya afya

16th May 2012
Print
Comments
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi

Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi 2007-17 (MMAM) na Mpango Mkakati wa Rasilimali Watu katika Sekta ya Afya 2008-2015, imeweka mikakati ya kuongeza kasi ya kuongeza watumishi katika sekta hiyo.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi kwenye uzinduzi wa kampeni ya miaka mitatu ya kuchangia fedha za mafunzo ya wakunga nchini, ili kuongeza wingi na ubora wa wakunga nchini na kupunguza vifo vya wanawake.

Aidha, alisema Wizara kwa kushirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Utumishi imekuwa ikiongeza idadi ya wataalamu wa afya wanaoajiriwa kila mwaka, ambapo mwaka 2011/12 watumishi zaidi ya 7,000 wameajiriwa.

Alisema mafunzo hayo ya ukunga yatakayotolewa kwa wataalam hao, yatasaidia kupunguza maambukizo mapya ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, kumuwezesha mkunga kumtibu mjamzito mwenye malaria kali, pamoja na kumhudumia mama nayetokwa damu sana.

Kwa upande wake mke wa Rais, mama Salma Kikwete, alitoa wito kwa wadau mbalimbali zikiwemo serikali za mitaa, mashirika ya maendeleo na taasisi za kijamii kuwekeza kwenye mafunzo ya wakunga, ili kupunguza tatizo la upungufu wa wataalam hao kwa asilimia 50, kwani idadi ndogo ya wakunga waliopo inawanyima kina mama fursa ya kupata huduma bora za uzazi.

Alisema uboreshaji wa hali ya afya ya uzazi nchini haiwezi kutegemea serikali na wahisani kutoka nje peke yake, bali ni jukumu la Watanzania wote.

Kampeni hii iliyoanzishwa na Shirika la kimataifa lisilo la kiserikali linaloshughulikia masuala ya tafiti na afya (Amref), kwa lengo la kuwapa mafunzo wakunga 15,000 barani Afrika, ambapo kwa Tanzania pekee wakunga watakaonufaika ni 4,222.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles