


Dereva Hamis Hussein (27), mkazi wa Vingunguti Mtakuja jijini Dar es Salaam amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa shtaka la wizi wa gari.
Alisomewa shtaka hilo na upande wa Jamhuri mratibu wa Polisi Kredo Rugaju na kusikilizwa na Hakimu Tarsila Kisoka.
Ilidaiwa mahamani hapo kwamba Januari 21 mwaka huu mtaa wa Lumumba Wilaya ya Ilala jijini hapa, mshatkiwa aliiba gari aina ya Nissan yenye namba za usajili T 483 BQM yenye thamani ya Sh. milioni 3.4 mali ya Fatuma Yusuph.
Hata hivyo, mshtakiwa alikana shtaka na amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana na kesi imeahirishwa hadi Julai 9, itakapotajwa tena.