Tuesday May 3, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Hukumu nyingine ya Maranda leo

17th May 2012
Print
Comments
Rajabu Maranda

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, leo inatarajia kutoa hukumu ya wafanyabiashara wawili Farijala Hussein na Rajabu Maranda wanaokabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi na wizi wa Sh. Bilioni  2.266 za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa).

Hukumu hiyo itasomwa na jopo la mahakimu watatu wakiongozwa na Fatuma Masengi ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania, aliyepewa kibali na Jaji Mkuu kusikiliza kesi hiyo, Projestus Kahyoza na Katarina Revocat.

Awali, shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Noel Shani aliifafanulia mahakama hiyo kwamba wamiliki halali wa jina la biashara la Kampuni ya Money Planers & Consultant ni Paul Nyingo na Fundi Kitunga.

Shani ambaye ni Msajili Msaidizi kutoka Wakala wa Majina ya Biashara (Brela), alidai kuwa washtakiwa Maranda na Hussein sio wamiliki halali wa jina hilo la biashara.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kuwa Machi 20 na Desemba 25, mwaka 2005 washitakiwa walijipatia ingizo la Sh. 2,266,049,041.25 wakidai kwamba Kampuni ya B. Graciel ya Ujerumani imehamishiwa deni na Kampuni ya Money Planers & Consultant ya Tanzania.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles