Saturday Apr 30, 2016
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia
Badilisha Lugha KISWAHILI

Mbunge wa Chadema azushiwa zengwe

15th May 2012
Print
Comments
Mbunge wa Viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Leticia Nyerere.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekanusha taarifa zilizozaa kwenye mitandao kuwa Mbunge wa Viti maalumu kupitia chama hicho, Leticia Nyerere, amekamatwa na uhamiaji kwa kosa la kukiuka masharti ya Green Card na kusema kuwa hayo ni majungu ya kukichafua chama.

Akizungumzia tuhuma hizo jana, Katibu Mkuu wa Chadema Taifa,  Dk. Willibrod Slaa, alisema  taarifa hizo ni za uwongo na hazina ukweli wowote ndani yake.

Alisema,amewasiliana na wanachama na wapenzi wa Chadema walioko ndani ya nchi na nje na kusema kuwa Leticia hajakamatwa.

Aliongeza kuwa, taarifa hizo zilizozagaa zinalengo la kukichafulia chama ndani na nje ya nchi kwa sababu wanachama wa chama hicho wanatarajia kufanya mkutano wao Washington DC Marekani siku chache zijazo.

“ Wanachama wa Chadema waishio Washington DC Marekani wanatarajia kufanya mkutano huko  na wabunge watatu kutoka nchini watakwenda kuhudhuria mkutano huo,” alisema Dk. Slaa.

Naye Leticia Nyerere, alisema kuwa  taarifa hizo si za kweli na anazikanusha vikali.

“Napenda kuchukua nafasi hii kukanusha vikali taarifa iliyosambazwa kupitia Jamii Forum kwamba  Leticia Nyerere amekamatwa. Kwa kweli hizi taarifa si za kweli. Ni za uzushi na kutaka kuchafuana.

Tunalaani vikali kwa mtu yeyote aliyehusika na kueneza taarifa hizi za kizushi zisizokuwa na msingi wowote,” alisemaLeticia Nyerere.

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment

Articles

No articles