Thursday May 23, 2013
| Text Size
[-]
[+]
Search IPPmedia

Simba yawashitaki Yondani, Yanga TFF

9th June 2012
Print
Comments
Kelvin Yondani

Uongozi wa Simba umesema umewasilisha kwa shirikisho la soka (TFF) malalamiko juu ya usajili wa mchezaji wake Kelvin Yondani kwa klabu ya Yanga.

Akizungumza na Nipashe jana, makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' alisema wamewasilisha malalamiko yao kimaandishi ofisi za TFF kupinga kitendo hicho cha Yanga.

"Ninachoweza kusema hiki kitendo kimetukera na kamwe hatuwezi kikuvumilia," alisema kiongozi huyo na kufafanua "Mwenyekiti wangu (Isamil Rage) jana aliwasilisha malalamiko kimaandishi kwa TFF.

"Tunataka wachukue hatua juu ya kitendo hiki cha kihuni kwa sababu huwezi kumsainisha mkataba mchezaji ambaye ana mkataba na klabu nyingine."

Alisema barua hiyo ya malalamiko wameiwasilisha TFF jana kuliomba Shirikisho hilo kuingilia kati na kutoa ufafanuzi na adhabu kwa wakosefu.

Kaburu alisema kuwa mpira una taratibu zake na lazima TFF izisimamie taratibu hizo na kutoa adhabu kwa klabu inayokwenda kinyume na taratibu hizo.

Alisema kuwa sakata hilo litafuatiliwa na kusimamiwa na Rage ambapo atahakikisha haki inatendeka na kanuni na sheria zinafuatwa.

Alisema Simba haina wasiwasi kuwa Yondani si mchezaji wake kwasababu "TFF wanautambua mkataba wetu mpya na Yondani (wa Desemba 23) maana baada ya kusaini naye tuliupeleka TFF na wakatugongea muhumuri kwenye kopi yetu ya mkataba kuonyesha wameupokea.

"Ushahidi huo tunao kwa sababu kopi ya mkataba ambayo imegongwa muhuri tunayo."

Yanga ilingiam kataba na Yondani ikidai makubaliano baina ya Simba na beki wa kati wa timu ya taifa huyo yalimalizika tangu Mei 30, mwaka huu.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alipiulizwa jana kama shirikisho hilo limepokea barua hiyo ya malalamiko ya Simba alisema hana taarifa kama imefika TFF.

Wakati huo huo, klabu ya Yanga imesema kuwa haina hofu juu ya usajili wa Yondani kwa kuwa wamemsajili mchezaji huyo kihalali baada ya mkataba wake na Simba kumalizika.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga aliyejiuzulu, Seif Ahmed, alisema Yondani amesajiliwa kihalali kwa kuwa alimaliza mkataba wake Simba.

Yondan anatuhumiwa kusaini mkataba sehemu mbili ambapo awali anadaiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu yake Desemba mwaka jana kwa dau la sh. milioni 25 lakini juzi akaingia na Yanga mkataba kwa sh. milioni 30.
 

SOURCE: NIPASHE
0 Comments | Be the first to comment